Mchipuko

Rwanda nayo yaruhusu kilimo na mauzo ya bangi

Rwanda nayo yaruhusu kilimo na mauzo ya bangi

Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa, imehalalisha kisheria ukulima na mauzo ya nje ya nchi ya mmea wa bangi kwa ajili ya matumizi ya tiba ili kupata fedha.
Kikao cha baraza la mawaziri kilichokaa Jumatatu kiliidhinisha “miongozo juu ya ukulima, usindikaji na mauzo ya nje ya mimea ya matibabu ya thamani ya juu nchini Rwanda ”.
Akizungumza na televisheni ya taifa hilo Jumatano hii Waziri wa Afya wa Rwanda Dkt. Daniel Ngamije alisema mimea hiyo inajumuisha bangi.
Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki limehalalisha bangi baada ya nchi kama Malawi, Lesotho, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe kuhalalisha kisheria mauzo ya bangi au matumizi ya mmea huo.
Waziri wa Afya wa Rwanda ameeleza kuwa, nchi hiyo inataka “kutoa mchango wake kwa vituo vya utafiti na sekta ya madawa kwa kutoa raslimali ili ipate faida ya fedha…”
Mwaka jana, soko la bangi la dunia lilidhaniwa kuwa na thamani ya dola bilioni 150 billion, kulingana na Benki ya Barclays.
Ni wakulima waliopewa leseni ambao wataruhusiwa kuzalisha zao hilo “uvutaji wa bangi bado unazuiwa ”, kulingana na bodi ya maendeleo ya Rwanda imesema taarifa iliyotolewa na serikali ya Kigali.
Iwapo utapatikana unalima au kuuza bangi nchini Rwanda unaweza kuadhibiwa hadi kifungo cha maisha jela, huku mvutaji akikabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela kwa mujibu washeria za nchi hiyo.

Soma hii pia ( mke wa bobby collymore aelezea maisha yake baada ya kifo Cha mumewe)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *