Maisha

Wambui kamiru aelezea maisha yake baada ya kifo Cha Bob collymore

Wakati Bob Collymore alipogundua kuwa ana ugonjwa wa saratani ya damu, alianza kupanga mazishi yake. Vile itafanyika, mda utakaotumika kwa kuendesha hiyo sherehe na zile nyimbo zitachezwa kwa mazishi.

Alipanga karibia kila kitu isipokuwa nguo yenye angevalishwa akifa. Mkewe ilibidi amchagulie nguo zake za safari ya mwisho ambapo alichangia nguo nyeupe bila Viatu Wala mapambo.

Bob collymore biography

Akielezea haya yote wakati wa ukumbusho wake jumatano iliyopita, wambui alisema alimpoteza mtu mhimu sana maishani na kifo chake kilibadilisha maisha yake

Wambui Kamiru ambaye ndiye aliyekuwa mke halali wa Collymore alieza safari ya kifo Cha mumewe mpaka alipoaga dunia. Anakumbuka vizuri mumewe akitetemeka na alidhania ako na malaria.

bob collymore wedding

Madaktari walijaribu kila juhudi na anakumbuka vizuri mumewe akidungwa sidano ili kuyapunguza makali ya ugonjwa wa saratani. Pia anakumbuka alivyokufa mpaka wakati mwili wake ulipochomwa na kuwa jivu.

Wambui kamiru and uhuru kenyatta

Tokea bob collymore aage dunia July tarehe moja mwaka Jana, wambui Kamiru alipoteza hisia ya harufu. Tokea siku hiyo tatizo la kutohisi harufu bado lipo. Mwezi wa March aliwahi ku tweet akiongezea hilo tatizo huku akisema ameishi miezi kadhaa akiwa na hilo tatizo.

Kwa sasa tatizo hilo laonekana kupotea na huenda hisia ya harufu ikamrudia.

“Ukiwa katika hali ya kuondokewa na kipenzi chako, vitu vingi hujitokeza. Unaweza patwa na tatizo la akili ama labda matatizo ya macho. Kufiwa ni Kama sumu iingiapo kwenye mwili wako na kuleta madhara ambapo kwangu ilidhuru hisia ya harufu…. Alisema wambui kamiru.

Bob collymore alikufa jumatatu na kufikia kesho yake, siku ya jumanne alikuwa ashafanyiwa mazishi ambapo watu kidogo ndio walioruhisiwa kuhudhuria. Alijulikana afrika mashariki na wengi walitegemea afanyiwe sherehe kubwa.

Hili halikufanyika maana yeye mwenyewe alitaka mazishi yake iwe hivo. Sio kusema tu, pia aliandika na kuhifadhi maandishi hayo ili akifa wahusika waweze kufuatilia alichotaka kufanyiwa.

“Maandishi yote yalikuwa kwenye kitabu na wakili wake aliweka sahihi ili yote aliyoandika yaweze kufwatwa…. Alisema wambui kamiru ”

Bob collymore alisema atakapokufa asije akawekwa na kuzungushwa kila sehemu maana ashamalizana na haya maisha ya hapa duniani

Mkewe aliongezea kuwa kuna jumbe zingine aliwachiwa marafiki zake wakiwemo Joshua oigara kutoka KCB, mtangazaji Jeff Koinange, mwanasiasa Peter Kenneth, muuza hisa Aly-khan Sachu, mkurugenzi wa scan group Bharat Thakrar na wengineo.

Marafiki wake walimsaidia wambui kamiru kwenye matayarisho ya mazishi ya bob collymore na kuhakikisha kila kitu kingekuwa shwari.

“nawashukuru wote walionisaidia wakati huo mgumu maana singeweza peke yangu…. Alisema wambui kamiru”

Alipojua kuwa ako karibu kuaaga dunia, Bob collymore alianza kuawaaga watu wake wa karibu akiwemo rais uhuru kenyatta.

Wambui kamiru and uhuru kenyatta

 

Aliwapanga kabisa watakaoongoza mazishi yake. Kwa mfano, bwana Bharat alichaguliwa Kama atakayeongoza uchomaji wa mwili wake naye Koinange na wenzake wakachaguliwa ili wahakikishe kila kitu kimefanyika kama alivyopanga.

bob collymore cars

Wambui kamiru aliwashukuru wakenya walio kuwa naye wakati mgumu huku akisema wengi kwake alikuwa hawajui kabla ya kifo Cha mmewe bob collymore lakini walijitokeza wakati huo kumsaidia.

Kuna wakati wambui kamiru alikuwa mkahawani Nairobi, wiki moja baada ya mmewe kufariki. Anakumbuka vizuri sana akilia. Alipofikia nyumbani alishangaa kupata ujumbe mfupi kwa simu yake uliosema;

“Nimekuona ukilia, nikafikiria nikuongeleshe ila roho ikaniambia nikuache…nataka ujue kuwa tuko pamoja na nakuombea kila siku….”

Wambui kamiru alisema mwenye kutuma ujumbe huo hawakuwa wanajuana kabisa na kuongeza kuwa hata wa leo hupokea jumbe kama hizo.

Hapo ndipo alipogundua kwamba, ni vizuri kuishi maisha ya kawaida bila kukwaza mtu yeyote maana atakaye kusaidia humjui.

kwake anaona Kama mmewe bob collymore alifariki miaka miwili iliyopita. Bob collymore aliweza kupigana na ugonjwa huu kwa mda na aliweza kufaulu Mara Kama mbili.

Mkewe bob collymore anaamini kuwa ugonjwa wa saratani unaweza ukapona. Bwanake alufaulu Mara mbili ila Mara ya tatu akalemewa. Anawahimiza wakenya waweze kula chakula Cha afya na wafanye mazoezi ili wawe na afya Bora.

Wambui kamiru alisema bob collymore hajawahi lazwa hospitalini anasema Mara ya mwisho kuwa hospitalini ilikuwa mwaka wa 2017 alipokuwa alikipimwa kama ana saratani ya damu. Bob collymore alikufa alikiwa na umri wa miaka 61.

Soma hii pia ( afya ya Raila odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *