Afya

Habari zaidi kuhusiana na afya ya Raila odinga

Wengi wamekuwa wakifuatilia mengi zaidi kuhusiana na afya ya Raila odinga

Kinara wa chama Cha ODM mheshimiwa Raila Odinga anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Saudi German Dubai
(SGH Dubai)

Raila Odinga news today
Raila odinga na Rais uhuru kenyatta

Raila odinga alifanyiwa upasuaji wiki hii baada ya kulazwa huko united Emirates

Msemaji wa familia ya odinga alieleza daily nation kwamba Raila odinga alikuwa yuafanyiwa upasuaji mdogo kwa mgongo ila haikuwa tatizo kubwa. Ijumaa, naibu wa chama Cha ODM bwana hassan Joho aliweza kutoa watu hofu baada ya kuongea na Raila odinga na kuhakikisha wanainchi kuwa Raila ako salama.

” Niliweza kuongea naye kiongozi wangu ambaye kwangu ni baba wa taiga na nilifurahia maana anaendelea vizuri na mda wowote atakuwa yuarudi hapa nchini…alisema joho

Hassan Joho aliwakumbusha watu kuwa wanasiasa ni Kama wanadamu wakawaida kwa hivyo pia wao huwa wagonjwa. Joho aliongezea na kusema kuwa chama za ODM kitazidi kusimama na kiongozi wao ambaye ni Raila odinga.

Msimamizi wa hospitali ya Saudi German hospital Dubai, Ms Semira Dikbas hakuelezea mda gani upasuaji ilifanyika na mda atakapoachiliwa Raila odinga kwenye hospitali hiyo.

afya ya Raila odinga: Raila odinga and Dr.Oburu Odinga

Jumatano, kakake mkubwa ndiye aliyetoa habari kuhusiana na aliko Raila odinga baada ya watu kuanza kuulizana kwenye mitandao

” Kakangu Raila odinga ako nje ya nchi kwa upasuaji lakini hali yake iko sawa.. alisema daktari Odinga.

Soma hii pia (utajiri wa Raila odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *