MaishaMchipuko

Daudi Anguka, Mtayarishaji wa tamthilia ya Pete amfuta machozi Lolani kalu

Daudi Anguka, Mtayarishaji wa tamthilia ya Pete amfuta machozi Lolani kalu.

Baada ya Lolani kalu kuangaziwa na vyombo vya habari, wengi walijitokeza ili waweze kumsaidia. Lolani kalu alikuwa mtangazaji wa runinga ya NTV kabla ya kupoteza kazi. Kwenye mahojiano na wanahabari, Lolani aliomba kusaidiwa na kamera na tarakilishi ili aweze kuanzisha  shirika la utangazaji.

Lolani kalu Daudi Anguka

Daudi Anguka ambaye ndiye mtayarishaji mkuu wa tamthilia ya Pete inayopeperushwa maisha magic alisikia kilio Cha Lolani kalu na kuamua kumsaidia ili aweze kujikimu kimaisha.

Katika ofisi za AR Films zilioko Nyali mombasa, Daudi Anguka alikumkabidhi camera na tarakilishi kama Kama alivyo ahidi hapo awali. Kwa sasa, wengi wamejitolea kumsaidia Lolani kalu na kufikia Sasa gwiji huyu ameuona mwanga baada ya kupitia magumu hapo awali.

Pete maisha magic Daudi Anguka

Hapa mwangaza tunamshukuru Daudi Anguka na wengineo waliojitolea kufanikisha ndoto za Lolani kalu.

Soma hii pia (Serikali ya uhuru kenyatta yakosolewa huku magufuli akisifiwa)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *