AfyaMchipuko

Pelosi ataka faili la hali ya kiafya ya Trump liwekwe wazi, Trump asema ni kichaa

Pelosi ataka faili la hali ya kiafya ya Trump liwekwe wazi, Trump asema ni kichaa

Spika wa Kongresi ya Marekani Nancy Pelosi amesema kuwa Wamarekani wana haja ya kujua hali ya kiafya ya Rais Donald Trump akiashiria maradhi yake ya virusi vya corona na kulazwa hospitalini kwa siku kadhaa.

Pelosi amewaambia waandishi habari kwamba, kuna swali muhimu ambalo Donald Trump anapaswa kulijibu nalo ni kwamba, alipima lini virusi vya corona na kupewa majibu ya kuwa salama kabla ya kupatwa na visuri vinayomsumbua kwa sasa na kukiri hadharani?

Spika wa Kongresi ya Marekani amesema kuwa, kuwekwa wazi swali hilo kutasaidia katika kujua hatua zilizochukuliwa baadaye.

Nancy Pelosi pia ametangaza kuwa leo Ijumaa atawasilisha muswada wa kuundwa tume ya kufanya uchunguzi kuhusu uwezo wa Donald Trump wa kuongoza nchi.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Spika wa Kongresi ya Marekani imesema muswada huo wa tume ya kuchunguza uwezo wa Rais wa kutekeleza majukumu yake ni katika fremu ya marekebisho ya 25 ya katiba ya Marekani ambayo inasisitiza kuwa rais wa nchi anapaswa kukabidhi madaraka kwa makamu wake pale hali yake ya kiafya inapomzuia kutekleza majukumu yake.

Donald Trump amejibu matamshi hayo ya Spika wa Kongresi ya Marekani kwa kumtaja Nancy Pelosi kuwa ni kichaa anayepaswa kuwekwa chini ya uangalizi.

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *