MchipukoSanaa

Serikali ya magufuli yasifiwa na msanii wa kenya huku akilaumu serikali ya kenya

Serikali ya magufuli yasifiwa na msanii wa kenya huku akilaumu serikali ya kenya. Sababu ya kufanya hilo ni kuwa msanii huyu kwa jina kalamoto amekuwa akifuatilia sanaa ya nchi jirani na anaziona jitihada za serikali ya magufuli. Kupitia facebook account yake, kalamoto alikuwa na haya ya kusema,

campaign ya serikali ya magufuli Chama Cha CCM

” Hatujifunzi kwa kuskia,basi kwa kuona pia.!Nchi Jirani wamekua na campaign za kisiasa takriban mwezi sasa,ila wanachofanya wanakaribisha wasanii wao kwenye jukwaa na kuburudika na miziki Yao.Ila ni tofauti sana na hapa kwetu.

Siku za campaign wanaitwa wasanii wa jamhuri tofauti kuja kutumbuiza kwenye majukwaa yetu kwa vigezo vya kua ni wasanii wakubwa..! Hata na ukubwa wa Sauti soul bado hawawezi kupata mwaliko.Kwanini?kwa sababu kila jimbo,kata,mtaa una wasanii wake wakuwakilisha mbali na wasanii maarufu tunaowajua..Hii inaonyesha upendo kutoka ngazi za juu na kufatilia mziki wa nyumbani kwa makini na kidemocrasia zaidi wa kizalendo

Ombi kwa taifa letu!!

Mziki sio uhuni tena umekua ajira ya vijana wengi,so ingekua vyema serikali ipitishe sheria na mswada ya kulipa kazi za msanii na ulipaji wa mirabaa(royalties) inavyostahili na kuzibiti vikali uwizi unaoendelea hapa nchini , vyenginevyo tutakuja kushindwa kuzuia moto iwapo wasanii watachoka na kuamua vyengine.

kalamoto kwenye tamasha la turnup
kalamoto kwenye tamasha la turnup

Inapata takriban miezi saba tangia hizi story za corona zianze.Sisi kama wasanii tuna maisha pia na tunategemea huu mziki wetu .Kama wazalendo wa nchi hii ingekua vyema tukumbukwe na kupangiwa mazingira ya kutafuta riziki ( we can still perform kwa kuzingatia sheria zilizoekwa ili mradi kuzuia usambazaji wa “ugonjwa” huu)

magufuli amvulia kofia diamond platnumz

Ikumbukwe vijana wengi waliacha uhuni na kujiunga na mziki kwa kuamini watajipatia riziki humu ..Sasa kama riziki hawapati hamuoni kabisa kurudi walivyokua zamani ni rahisi sana.Tuilinde nchi yetu kwa kugawa nafasi sawa kwa wote.’Zile show za mitandaoni na kulipwa kwa wasanii hakujafika kwa wote..

Kama viongozi wanaweza kuandaa mkusanyiko wa maelfu ya watu mbona isiwe wasanii kuandaa shows wenye maelfu ya mashabiki..We are also leaders in our music plus we all the shame hata na common mwananchi.So pity,inawalazimu wasanii kwenda nchi za nje kutumbuiza kana kwamba hawana nchi yao na mashabiki kwenye nchi hiyo.Sawa watu kama Eric omondi wataweza kisa wana mashabiki nchi zile,jee umejiuliza wale wasanii ambao hawana majina au kazi zao hazijavuka mipaka wanakula wapi kipindi hichi chote.!!

campaign ya serikali ya magufuli Chama Cha CCM

Nchi zengine zinaendelea na maisha na Hali ya kila siku kwa kuzingatia sheria za nchi husika..Vile vile pia sisi tunaomba kurudi kwa Hali ya kawaida ,tutafute suluhu ya haraka.! Kisa wanafunzi mlowapa nafasi kua nyumbani nao,kumekua na ripoti za kutatanisha (wanafunzi wengi hususan wa kike wamepata uja uzito na wengine kuolewa ingawa wadogo.Elimu kutupwa kando,na masikitiko yangu ni kua tutapoteza nguvu kazi ya taifa.)..”

Msanii huyu ashawahi kurekodi nyimbo akilaumu nchi yake kwa kutoangazia wasanii wake sanasana wa mziki wa hip-hop. Hana uwoga na anachotaka kusema huwa hazuiliki na akiamua hata azuie nani atasema tu. Basi ukiona imefikia hatua ya kusifu serikali ya magufuli,Basi ujue kuna tatizo sehemu flani.

Soma hii hapa ( wasanii wa kenya na masaibu wanayoyapitia)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *