MzikiSanaa

Wasanii wa Kenya

Kenya ni nchi ya kipekee sana na tunaweza sema kuna wasanii wengi sana. Wasanii wa kenya wanajulikana maeneo mingi ulimwenguni ila sio wote wako na nafasi ya kuifurahikia biashara ya mziki. Mziki wa Kenya unasemekana kudhibitiwa na watu tofauti wanaojiita cartel. Wasanii wa kenya hunyimwa nafasi kwenye matukio mbalimbali kwa kukosa watu wa kuwaunganisha na wamiliki wa sanaa hapa nchini kenya.

Wasanii wa kenya wanaochipukia hupitia wakati mgumu sana. Hii ni kwa sababu wanaotakikana kuwashika mkono hujifikiria wao tu na kila dili wanaoipata hujiweka wao kwanza huku wakiwasahau wasanii chipukizi. Hii ndio sababu sanaa ya Kenya ipo tofauti na sanaa ya nchini Tanzania. Wasanii wa Tanzania husaidiana zaidi na msanii akipatikana ana kipaji, basi atapata usaidizi mkubwa sana kutokana kwa wasanii wenzake.

Ifuatazo no Orodha ya wasanii wa Kenya wenye majina yao kidogo inajulikana hata nje ya nchi ya Kenya. Kwa sasa tunaweza sema Kenya inajivunia wasanii wengi tajika kuliko miaka ya hapo Mbeleni.

Masauti

Masauti wasanii wa kenya

Masauti ni msanii anayefanya vizuri sana kwa sasa. Msanii huyu ni mzaliwa wa pwani. Kabla ya kuona mwangaza, Msanii huyu ameteseka vya kutosha. Aliwahi kuwa chini ya usimamizi wa Teddy Josiah. Usimamizi huu haukuzaa matunda kwani Teddy Josiah alimpeleka njia ambayo sio. Kulingana na wengi, Teddy Josiah alitaka kutengeneza aina flani ya mziki “Swahili RNB lakini haukuridhisha wengi hivo kuadhiri talanta ya Masauti. Baadaye msanii huyu alijikuta kwa mikono ya Jblessing ila pia hakunufaika inavyostahili. Baadaye alikutana na meneja anayesemekana kuwa na hela nyingi aliyeamua kusimamia kazi za masauti. Bila shaka meneja huyu alifanikisha juhudi za masauti na kwa sasa masauti ako vizuri na anajulikana ulimwengu mzima.

Khaligraph Jones

Khaligraph Jones with a shot gun

Ni mzaliwa wa kenya ila ukisikiza nyimbo zake kwa makini sana utadhania kazaliwa ulaya. Khaligraph jones hujiamini sana na anamini yeye ndiye msanii bora zaidi Nchini kenya. Haogopi yeyote na wakati anapoandika nyimbo anaweza akaamua kumpasha mtu kwenye verse bila kujali Kama mwenye kutajwa atakasirika ama la. Unapotaja wasanii wa Kenya, Khaligraph jones lazima atakuwa kwenye hiyo Orodha.

King Kaka / Kaka Sungura

King Kaka Kaka sungura

Ni msanii anayesemekana kuwa na bidii ya Mchwa. Amesajili wasanii ndani ya label yake na wote wanafanya vizuri katika sanaa ya mziki. Aliwahi kusajili Rich Mavoko kutoka nchi ya Tanzani kabla ya msanii huyo kuchukuliwa na wasafi Records. Kumbuka King Kaka ndiye msimamzi wa msanii wa kike kwa jina Femi one aliyegonga vyombo vya habari na nyimbo ya ” Utawezana”

Nyimbo yake ya wajinga nyinyi iligonga vyombo vya habari. Kwenye nyimbo hiyo aliwapasha wanasiasa mashuhuri kama vile Waiguru na hata ikasemekana alitakikana kufika kituo cha polisi kuandikisha ripoti kuhusiana na nyimbo hiyo. Waliotajwa kwenye hiyo nyimbo walidai kuchafuliwa majina yao huku wakiongezea kuwa nyimbo hiyo haikuwa na ukweli wowote. Wengi walisima na King kaka wakiwemo wanasheria na kufanya wanasiasa waliotaka King kaka ashikwe kuingiza baridi na kuamua kuachana na hiyo kesi.

Otile Brown

Otile brown wasanii wa kenya

Kama wanavyosema, Msanii huyu ni kipenzi cha warembo. Aliwahi kuwa chini ya Docta Eddy ila kulizuka sitofahamu na wawili hawa wakaamua kuachana kiroho safi. Docta Eddy alizitoa video za Otile brown kwa youtube na kumkataza msanii huyu kutumia hizi nyimbo hizo kwa tamasha yoyote. Baada ya mda msanii huyu alifungua youtube channel mpya na kuanza kueka tena kazi zake mpya. Kwa sasa Youtube ya Otile brown inafanya vizuri kwani ina watazamaji wengi sana hata kuliko nwakati alikuwa chini ya Docta Eddy.

Size 8

Size 8 ni msanii wa gospel. Kabla ya kujiunga na secta ya gospel, Size 8 alikuwa anafanya nyimbo za kidunia. Aliwahi kusema kuwa wakati alikuwa kwa secular music hakuwahi kuwa na furaha ila kwa sasa vile ako kwa mziki wa injili anaweza akatabasamu. Msanii huyu wa kike ni kati ya wasanii wa kenya waliofanikiwa zaidi. Kwa sasa ako kwa uhusiano na Dj Mo ambaye anafanya kazi Nation Media kama Dj wa nyimbo za injili kwenye kipindi cha Crossover kinachokujia Ndani ya NTV kila jumapili.

Avril

Ni msanii wa kike ambaye alikuwepo tangu hapo mwanzo. Kwa sasa anasemekana kuwa kwa uhusiano na J blessing ambaye ni mwelekezi wa Churchill show. J. Blessing aliwahi kuwa kwa uhusiano mwingine ila aliachana na mwanadada huyo. Kwa sasa wawili hawa wamefanikiwa na mtoto mmoja. J. Blessing ndiye anayesimamia kazi zote za Avril kwake ni kama meneja wake.

Susumila

Susumila na Ommy dimples

Ni msanii anayetokea county ya Mombasa. Anaoekana kuwa na bidii sana kwenye sanaa ya mziki. Amefanya colabo na wasanii wengi wa Bongo akiwemo Mbosso, Lavalava na Ommy Dimples. Huwa ni mkaribu wa Gavana Hassan Joho na inasemekana anapata usaidizi mkubwa sana kutoka kwa Gavana wa Mombasa Hasssan Joho. Ni mmoja wa wasanii wa mombasa ambaye ameweza kupenya hadi nchi jirani ya Tanzania.

Willy Paul

alaine and willy paul

Unapotaja wasanii wa kenya, utajikuta umemtaja msanii huyu. Willy paul alikuwa msanii wa injili ila kwa sasa ameamua kuiaga hiyo secta na kuamua kufanya mziki wa mapenzi. Kulingana na yeye, Mziki wa injili nchini Kenya umejaa fitina na wengi hawapendi maendeleo ya wasanii wenzao. Alisema wengi walishikana na watangazaji wa radio pamoja na runinga na kuamua kugomea Nyimbo zake. Kwa sasa msanii huyu anadai tangu achane na mziki wa injili ameanza kufanya dili nyingi kwani hakuna kinachomzuia kufanya anachokitaka. Yetu hapa mwangaza news ni macho tu.

Bahati

Bahati and diana

Khaligraph Jones humuita mtoto wa Diana. Diana ni Mke wake na wawili hawa huonekana kutoogopa yoyote kwani mapenzi yao huyaweka wazi kwa mitandao bila uoga wowote. Bahati ni msanii wa pili kugomea mziki wa gospel baada ya Willy Paul. Ashawahi kuwa na kipindi chake kwa jina Being bahati alichomshirikisha Diana Marwa ambaye ni mkewe. Kipindi hichi kilisimamishwa baada ya mda ila kwa sasa kinapatikana kwa youtube.

Timmy T Dat

Timmy T dat

Kama kuna msanii mwenye ni vigumu kumuelewa ni Timmy T Dat. Video zake zataka moyo kuzitazama kwani kama uko karibu na watoto wadogo ama wazazi, basi huenda ukajutia. Kuna video aliwahi kufanya na Rosa Ree ambayo haiukuchukua mda kabla ya kufungiwa na Ezekiel Mtua kwa kusemekana kutozingatia maadili ya jamii. Ni msanii ambaye amefanya colabo nyingi sana na wasanii wa hapa nchini kenya na Tanzania kwa jumla.

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *