Utawezana : femi one na mejja yazidi kupaa
Wanasema kitu ikiongelea kwa uzuri au kwa ubaya huzidi kupata umaarufu. Utawezana yake femi one na mejja ni mojawapo ya zile vitu zinaongelewa sana nchini kenya. Wasanii hawa wawili wafaa wapewe tunzo kwani kupitia mziki wao, wakenya wanapata burudani mpaka wamesahau janga la corona.
Wengi wamejitokeza kuikashifu nyimbo hiyo ya utawezana ila bado inazidi kuwa katika vinywa vya watu. Kwa sasa imefikisha millioni tatu katika youtube
Juzi ezekiel mutua ambaye anasimamia filamu hapa nchini kenya aliikashifu nyimbo hiyo akidai haina mafunzo yoyote kwa jamii. Jambo hilo halikuchukuliwa vizuri na wanainchi kwani wengi walidai hiyo nyimbo sio lazima kila mtu asikize. Meneja wa femi one pia aliweza kutetea madai ya ezekiel Mutua na kusema nyimbo hii imeweza kuleta furaha kwa wanaichi ikizingatiwa kuwa wanapitia wakati mgumu kwa sababu ya corona. Pia meneja huyo aliongezea na kusema japo anafahamu bidii ya Ezekiel mutua pia anafaa awape nafasi wasanii katika ubunifu wao.
Pia unaweza soma ( Utajiri wa diamond platinumz)
4,026 total views, 1 views today