Sanaa

Muigizaji Brian Ogola amejiunga na tamthilia ya Selina

Muigizaji Brian Ogola amejiunga na tamthilia ya Selina. Selina ni Tamthilia iliyoshinda tuzo za kalasha katika kitengo Cha “Best Swahili telenovela” mwaka Jana huku Tokodi akishinda muigizaji bora.

Selina hupeperushwa ndani ya maisha magic east na maisha magic plus chaneli zinazomilikiwa na kampuni mnet. Na ukitaka kuitazama hakikisha kila siku ya wiki saa mbili na nusu uko karibu na runinga yako.

Tamthilia hii inaangazia wapenzi wawili, Nelson ambaye kwa jina kamili Anajulikana kama pascal tokodi na Selina ambaye jina yake kamili ni Celestine Gachuhi.

Brian Ogola alianza kuonekana siku ya jumanne baada ya kuchukua nafasi ya reagan Makenzie. Katika tamthilia ya Selina, reagan Makenzie ndiye mtoto mkubwa wa familia tajiri ya makenzie.

Brian Ogola selina

Brian Ogola sio msanii wa kwanza kuigiza kama reagan, nafasi hii pia iliweza kuchezwa na marehemu Kone aliyefariki kwa ajali ya barabara.

Reagan ni mtu ambaye hapendi kuongea mengi. Katika familia ya Makenzie, Reagan hupenda kuvaa kivyake ila mke wake Zoe Makenzie ni mkali kiaina na Mara nyingi ndiye anayemfanyia maamuzi.

Brian Ogola poacher

Brian Ogola hivi majuzi aliigiza kwa sinema ya “Poacher” inayoonyesha Netflix, kampuni inayojulikana duniani kwa kulipa waigizaji hela ndefu. Sio poacher peke yake, muigizaji huyu ashawahi kuigiza kwa sinema zaidi

Soma hii pia ( jinsi azziad Nasenya alivyojiunga na selina )

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *