Sanaa

Mfahamu azziad Nasenya vizuri na jinsi alivyojiunga na selina

Azziad Nasenya anayejulikana kama queen of TikTok alijiunga na TikTok 2018. Anapenda kudance na kuiga nyimbo za watu ama kwa kimombo “lip-syncing”. Alipojiunga na TikTok hakudhania kuwa angefika pale alipo kwa sasa.

Aliwahi ku dance video ya nyimbo ya femi one na mejja “utawezana” ambapo kwa sasa imefikisha views milioni nne na zaidi.

Azziad Nasenya utawezana

Azziad Nasenya alizaliwa mumias na kusomea shule ya lugulu boarding school mpaka darasa la tatu kabla ya kuhamia Nairobi. Alipomalizia shule ya msingi, Nasenya alijiunga na st. Cecilia secondary school ilioko misikhu. Akiwa shuleni humo, Nasenya alijiunga na drama club iliyoshinda katika drama festival.

Alipomalizia shule ya upili, Nasenya alijiunga na kampuni ya hearts of arts ilioko Nairobi. Kiongozi wa kampuni hiyo alikuwa mwalimu wa misikhu girls na ndio ikawa rahisi kwa azziad Nasenya kujiunga nao. Tokea wakati huo, azziad Nasenya amecheza kwa sinema saba tofauti.

Azziad Nasenya tribe and age

Kwa sasa azziad Nasenya anasomea utangazaji katika shule ya utangazaji ya Kenya institute of mass communication.

Mara ya kwanza kwake kuonekana kwa runinga ilikuwa mwaka wa 2018 kwa tamthilia fupi kwa jina “parenting” iliyofanywa na kampuni ya film lab Kenya. Mwaka huohuo alipata nafasi katika tamthilia ya “MaEmpress”, tamthilia yenye ilikuwa ikipeperushwa ndani ya maisha magic east.

Katika Selina, azziad Nasenya ni rafikie Erico. Walikutana na nelson wakati alikuja kumtembelea Erico. Chichi ambaye jina lake halisi ni azziad Nasenya, alifikiria  nelson ni mhalifu aliyetaka kumvamia Erico.  Chichi aliweza kumkabidhi na kumfunga mikono lakini Erico anatokea na kumueleza chichi kuwa nelson sio mhalifu na hapo ndipo chichi anamfungua mikono. Watatu hawa wanatafuta njia ya kumaliza Messina.

azziad nasenya and selina nelson pascal tokodi

Vitu vitatu vyenye hujui kumhusu azziad Nasenya

  1. Ni mpishi Bora na anajua kupika chakula aina nyingi
  2. Anapenda sana usingizi na mda mwingi utamkuta amelala.
  3. Japo wengi wanamuonea Kama anapenda sana kuongea na kuzurura, mda mwingi hubakia ndani ya nyumba

alianza kuigiza akiwa darasa la pili

Alizaliwa wa kwanza katika familia.

Kumjua zaidi azziad Nasenya, “chichi”iiii ,ma tamthilia ya Selina kila siku ya wiki kuanzia jumatatu hadi ijumaa saa mbili na nusu ndani ya maisha magic east na maisha magic plus.

Soma hii pia (kutana naye director wa tamthilia ya Pete)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *