Maisha

Shix Kapienga, masomo, umri na mengi zaidi kumuhusu

Shix Kapienga ana talanta zaidi ya moja. Ni muigizaji na pia ni mtangazaji. Jina lake kamili Anajulikana Kama Nancy wanjiku karanja. Yuko tofauti na wakenya wengi na huishi maisha ya kivyake. Shix Kapienga anapenda reggae sana. Hupenda kuongea sheng’ wakati ako radioni na pia huiga waamerika wanavyoongea.

Umri wa shix Kapienga

Mwanadada huyu ana miaka thelathini na tatu.. alizaliwa kangemi Nairobi mwaka wa 1987 na amezaliwa akiwa watatu katika familia ya watoto wanne.

Masomo

Inasemekana shix Kapienga alikuwa wale watoto wenye husumbua kwa familia. Wakati wa mvua, alipenda kuchezea matope na kujichafua. Alipenda ule mchezo wa kalongolongo wakati tv station ilikuwa moja tu amabyo ni KBC. Maisha yake huko kangemi ndio ilimfanya awe muigizaji gwiji.

Shix Kapienga alisomea shule ya msingi ya Westlands primary school lakini baadae akahamia Samaritan primary school alipofanyia mtihani wa darasa la nane; KCPE. Baada ya kumaliza mtihani wa darasa la nane, alijiunga na shule ya upili ya mirithu girls high school ila baadae alihamia kangaru girls high school alipofanyia mtihani wa mwisho wa shule ya upili.

Baadae alijiunga na Daystar university alipozikwa utangazaji

Shix Kapienga michezoni

Alianza kujihushisha na michezo akiwa shule ya msingi. Alikuwa mchezaji mzuri sana wa volleyball. Wakati alikuwa shule ya kangaru girls, shix Kapienga na wenzake walifika provincial level. Michezo miingine aliwahi kujihushisha nayo ni pamoja na tennis, football, basketball, netball

Wakati bado akiwa shule ya upili, alijiunga na kikundi Cha uigizaji. Talanta ya uigizaji aliiendeleza alipomalizia shule ya upili baada ya kujiunga na theatre club. Mwaka wa 2008 alijiunga na ghetto radio akiwa mtangazaji katika secta ya michezo.

Jina ya shix Kapienga ilitokea wapi?

Jina hili alipewa na mtangazaji mwenza Mbussi wa radio Jambo. Kulingana na Mbussi shix ilitokana na ufupisho wa jina wanjiku. Kapienga ilitokana na tabia yake. Shix ni ufupisho wa shixx, neno la sheng’.

Katika filamu ya shuga’ alicheza Kama “baby” mwenye alidhulimiwa kimapenzi na mtu wa familia yake. Pia aliigiza kwa sinema ya Nairobi halflife. alipata nafasi pia Kama mwanamke wa kujiuza usiku. Japo wazazi wake hawakufurahia, filamu hii ilimfungulia milango na jina lake likawa kubwa afrika mashariki. Wazazi wake walikataa kuitazama hii movie mpaka wa leo. Aliwahi pia kucheza tamthilia ya bebabeba Kama Tasha.

Kazi ya utangazaji

Amekuwa mtangazaji wa hot 96 radio kwa mda ila habari zinazotufikia ni kuwa yeye na wengine walisimamishwa kazi na kampuni ya royal media inayoongozwa na sk macharia. Hotzone show yenye alikuwa yuaiongoza pamoja na mwenzake rapcha the scientist ilikuwa na umaarufu sana kwani zaidi ya watu million mbili walikuwa wanaiskiza. Inasemekana pia ni mwandishi wa kahawatungu website inayomilikiwa na Robert alai.

Uhusiano wa kimapenzi na mc Jessy

Gazeti moja la nairobian liliwahi kuandika kwamba shix Kapienga ako na uhusiano na mc Jessy wa Churchill show. Kapienga alikanusha madai haya alipouliziwa na kalekye Mumo na kusema anapenda kuishi maisha yake bila kutangaza. Aliwahi kuuliziwa Tena ndani ya ebru tv na akaapa kuivamia tv station hiyo Kama wataendelea kuzungumizia Hilo swala la uhusiano wake na mc Jessy.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *