Mchipuko

Muigai Njoroge alijikuta matatani sababu ya nyimbo yake mpya “ino migunda”

Muigai Njoroge ambaye ni mwanamziki wa nyimbo za kikuyu ametakiwa kufika mbele ya shirika la NCIC (national cohesion and integration commission) sababu ikiwa, nyimbo aliyoachia hivi karibuni ijulikanao kama “ino migunda”

Barua aliyopokea kutoka kwa shirika Hilo ilidai kwamba nyimbo yake mpya inasemekana kuwa na maneno yenye tishio na huenda ikahatarisha maisha ya jamii tofauti.

Muigai Njoroge anatakiwa kufika kwa shirika la NCIC June tarehe 26 kwa ofisi zao zilioko upper hill Nairobi. Asipofika atafunguliwa mashtaka na mahakama kuu ya Kenya

Kwa sasa nyimbo hiyo ya muigai Njoroge imefikisha views laki sita kwa YouTube. “Ino migunda” inaongelea vile maskini wanavyonyanyaswa na wenye wako kwa mamlaka.

Nyimbo hii inazidi kueleza kuwa watu walipigania uhuru ili wapate mashamba lakini kwa sasa mambo ni tofauti maana mashamba yenyewe yanamilikiwa na wachache.

Nyimbo hii inaendelea kuwaonya viongozi wanaopata mamlaka kupitia urithi huku mwanamziki huyu akionya kuwa siku moja yote yatakwisha na itakuwa mwisho wao

” Kuna siku mwanainchi wa kawaida atakata tamaa ya kunyanyashwa….*

Pia anaongelea swala la wanainchi walibomolewa majumba huko kariobangi. Muigai Njoroge anasema hii ilikuwa ni kinyume na ubinadamu ikizingatiwa kuwa walitolewa kwenye hizo nyumba wakati wa janga la Corona. Kulingana na yeye wangewastili mpaka corona iishe bila kusahau mvua kubwa iliyowanyeshea usiku huo.

Soma hii ( Tazama familia ya Anne Waiguru)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *