Mchipuko

Jalango asimamishwa kazi milele fm

Jalango ambaye alikuwa ni mtangazaji katika radio ya milele fm amepata pigo kubwa baada ya kusimamishwa kazi.

Sio yeye tu ila kuna watangazaji wengi wamejikuta pabaya baada ya mediamax kuamua kusimamisha wafanyi wake kazi na kudai biashara yao imeshuka kwa sababu ya janga la Coronavirus.

Kulingana na jalango, hataweza kuwa pale tena na ametoa shukrani zake kwa wafanyi kazi wenza na kuwatakia kazi njema. Ni juzi tu Betty kyalo alitangaza kuacha kazi K24TV na kuanzisha YouTube channel yake. Mpaka sasa Betty kyalo hajajiunga na station nyengine.

Kulingana na jalango, kuna vitu hawakuelewana kuhusiana na Sheria za kazi katika station hiyo yakiwepo malipo. Kwa sasa amehimiza wafuasi wake waweze kupatana kwa YouTube channel yake

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *