Maisha

Zari Hassan azua gumzo kuhusiana na umri wake

Zari hassan sio mwanamke wa kwanza kuwatatiza watu kuhusiana na umri wake kwani Hamisa Mobetto ashawahi kujipata katika hiyo hali.

Unapoongelea umri kwa mwanamke yeyote huenda ukazua gumzo. Sababu ni kwamba wanawake wengi hawapendi kujulikana miaka yao sanasana wakati umri wao umeenda sana.

Zari Hassan ilibidi juzi ajitetee kuhusu umri wake wakati passport yake ilivunja kwa mitandao na ikajulikana alizaliwa 1978

Kulingana na zari Hassan, hii ilikuwa njia ya kumuezesha kupata uraia wa nchi ya Afrika kusini. Ili kupata kibali Cha kusafiri, ilibidi aweze kuongeza miaka.

Alisema wengi wanamuonea wivu maana wanashangaa anavyopendeza na ako na umri wa miaka 38. Wanajaribu kivyovyote kuongelea umri wake ili waweze kumpoteza

“Naona kila mtu ana post passport yangu inayoonyesha kuwa nilizaliwa 1978, hiyo iko hivo kwa sababu ya kutafuta uraia wa afrika kusini ila Mimi nilizaliwa mwaka wa 1980.. wote mnaonichukia mko chini sana na kwa taarifa yenu nitazidi kuwa mrembo ata nikifisha miaka hamsini ama mia. Nitazidi kuwa mrembo kuliko nyinyi mliokosa hela…. Angalia ninavyo tesa nafsi za wengi na Niko peke yangu… Lakini ni sawa maana hata Mimi ningekuwa nyinyi ningemchukia huyu zari Hassan…….”

Zari hajawahi ongelea umri wake japo wengi husema mwanamke huyu ana miaka zaidi ya 40. Umri wa Zari hassan umekuwa gumzo tokea ile siku alianza uhusiano akiwa na miaka thelathini wakati diamond alikuwa na miaka ishirini na nne.

Wanawake huogopa sana kujulikana miaka yao kwani wengi huamini wanaume hupenda wanawake wenye umri wa chini.

Hamisa Mobetto age

Mwaka wa 2019 Hamisa Mobetto alijikuta na kesi kama hiyohiyo ya Zari Hassan baada ya gazeti moja ya Tanzania ku post kibali chake cha kuzaliwa. Kulingana na gazeti Hilo, ilionyesha wazi kuwa Hamisa Mobetto alizaliwa 1991 ila yeye hapo mbeleni alidai kazaliwa 1994.

Soma hii pia ( je Rayvanny anajiondoa WCB?)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *