Afya

Baada ya kuzaa | Maswali na majibu

Kuna matokea kadhaa hutokea baada ya kuzaa. Hii hutokea mda michache tu kabla ya mwanamke kujifungua.

Kati ya mambo yanayotokea baada ya kuzaa ni Kama vile

  • Hedhi baada ya kuzaa
  • Uke baada ya kuzaa
  • Mimba baada ya kuzaa
  • Tumbo kuuma baada ya kuzaa
  • Kufungwa tumbo baada ya kuzaa
  • Mtoto kulia baada ya kuzaliwa
  • Tendo la ndoa baada ya kuzaa
  • Kupunguza tumbo baada ya kuzaa
  • Damu kutoka baada ya kuzaa

Ningependa tuyapitie haya matokea yote ndio tuweze kuelewa tunachostahili kukifanya chochote kile kitatokea baada ya kujifungua.

Kupunguza tumbo baada ya kuzaa

Kawaida mwanamke anapokuwa mja mzito, huongeza uzani na pia tumbo lake hunenepa. Wanawake wengi wanachukia unene huu na hufanya kila njia ili kurudia Hali yao halisi. Jambo la kushangaza ni kwamba, kuna wanawake ambao hata bila kufanya lolote, shepu yao hurudi kawaida baada wa wiki kadhaa bila hata kutumia chochote.

Ili kupunguza tumbo, wanawake wengi huanza mazoezi inayowasaidia kuikaza ile tumbo na kuirudisha sehemu yake ya kawaida. Kumbuka pia chakula unachotumia kinachangia pakubwa mno kupunguza tumbo lako. Ila usije ukajinyima chakula ukasahau kwamba mtoto anategemea maziwa yako inayotokana na chakula unachotumia.

Tendo la ndoa baada ya kuzaa

Kulingana na mtandao wa  open.edu Baada ya kuzaa, Mwanamke anaweza kuanza tena kushiriki ngono iwapo lokia imekoma, uke na vulva zimepona, hana maumivu na yuko tayari kihisia. Hali ya mwili kuwa tayari kwa kawaida huchukua takribani muda wa majuma matatu hadi matano. Hata hivyo, mwanamke huyo anaweza kuchukua muda mrefu kabla ya kujisikia kuwa tayari kushiriki ngono na basi hapaswi kulazimishwa kukubali. Jukumu lako ni kuzungumza kwa upole na mwenzi wake ili kuhakikisha kuwa anaelewa na kuheshimu hisia za mwanamke huyo. Katika jamii nyingi kuna desturi inayothibiti wakati ambapo ngono inafaa kurejelewa na mara nyingi huwa baada ya puperiamu kuisha ambayo huwa baada ya majuma sita tangu kuzaa.

Uke baada ya kuzaa

Uke uliopanuliwa sana ili kumruhusu mtoto kupita hunywea pole pole ukirejea katika ukubwa na hali yake ya kawaida ilivyokuwa kabla ya ujauzito kwa kipindi cha takribani wiki tatu baada ya kuzaa. Kufikia wakati huu, upitaji zaidi wa damu na kuvimba kwa uke na vulva kunapaswa kuwa kumedidimia.

Hedhi baada ya kuzaa

Wakati wa kuanza kwa hedhi kwa mwanamke anayenyonyesha ni wa kubadilika sana na hutegemea vipengele kadhaa vikiwemo ni kwa kiasi kipi na ni mara ngapi mtoto huyo hulishwa, na ikiwa chakula hiki kimeongezwa maziwa bandia. Ovulesheni husitishwa kwa mwanamke anayenyonyesha na homoni itolewayo kwenye tezi ya pituitari iliyo ubongoni mtoto anaponyonya. Nusu hadi theluthi tatu za wanawake wanaowanyonyesha watoto wao pasipo kuwapa vyakula vingine vyovyote huanza kipindi chao cha kwanza cha hedhi katika majuma 36 baada ya kuzaa.

Tumbo kuuma baada ya kuzaa

Hii huwa sio kawaida sana kwa wanawake wengi ila hutokea. Huenda kuna hitilafu lakini ni vizuri kuchukua mda kabla hujafanya uamuzi wa kumuona daktari kwani wakati mwingine huwa ni uchungu wa dakika kadhaa alafu uchungu unaenda. Uchungu ukizidi unafaa umuone daktari ili aweze kukushughulikia na kukupa tiba inayostahili.

Damu kutoka ama kuvuja baada ya kuzaa

Takriban wanawake 127,000 kote duniani hufa kila mwaka kutokana na kuvuja damu baada ya leba na kuzaa. Hali hii hujulikana kama kuvuja damu baada ya kuzaa. Hali hii ni kisababishi kikuu cha vifo vya kina mama vinavyohusiana na kuzaa, nayo husababisha robo ya vifo vyote vya kina mama vinavyohusiana na kuzaa. Kila mwaka, visa milioni 14 vya kuvuja damu hutokea wakati wa ujauzito na kuzaa. Hali hii hutokea mara nyingi kwa sababu uterasi haikujikaza vyema baada ya plasenta kutoka. Katika Kipindi cha 6, ulijifunza kuhusu jinsi ya kudhibiti awamu ya tatu ya leba. Awamu ya tatu ya leba huanza kwa kuzaliwa kwa mtoto na kukamilisha kutoa kwa plasenta na membreni za fetasi.

Mtoto kulia baada ya kuzaliwa

Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.

Kufungwa tumbo baada ya kuzaa

Ni njia wanaotumia baadhi ya wamama na wanasema njia hii inasaidia kupunguza unene wa tumbo. Kufunga tumbo kunasaidia kuregesha shepu ya tumbo kama ikivyokuwa hapo awali kabla ya kuwa mja mzito. Kumbuka mtoto anapozaliwa kuna ile nafasi ya tumbo hubaki wazi na isipofanyiwa maarifa, basi mwanamke ataonekana kuwa na tumbo kubwa maana hiyo nafasi aliyekuwa mtoto itajaa mafuta.

Soma hii ( je kuna hatari ya kutofanya tendo la ndoa kwa mda mrefu)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *