HistoriaMaisha

Historia ya Ibraah : Maisha ya Ibraah

Wengi wanamfahamu Ibraah ila sio wengi wanaojua mengi kuhusiana naye kama vile mwaka  alipozaliwa majina yake Kamili na mengi kuhusiana na historia yake. Ifuatayo ndiyo historia ya Ibraah.

Kwa majina kamili, Ibraah anajulikana kama Ibrahim Abdallah Nampunga. Ni msanii chipukizi ila anafanya Kazi nzuri na ni mmoja wa wale wasanii wanaotegemewa sana katika soko la mziki wa Tanzania. Ako chini ya konde music worldwide inayoongozwa na Harmonize.

Ibraah ana miaka mingapi

Ibraah alizaliwa tarehe 3 mwezi wa July mwaka wa 1998 ndani ya hospitali ya temeke mjini Dar es salaam Tanzania. Kwa sasa (mwaka wa 2021) ako na miaka 24.

Masomo ya Ibraah

Ibraah alisomea shule ya Lukokode primary school iliyoko Tandahimba, mtwara. Alisoma Kati ya mwaka wa 2005 mpaka 2011. Ibraah hakuweza kuendelea na masomo zaidi kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kulipa karo ikizingatiwa kuwa tayari walikuwa wakimfundisha Idrissa Abdallah ambaye ni kakake Ibraah.

Baada ya masomo ya shule ya msingi, Ibraah alianzisha biashara ndogo ili aweze kuyasukuma maisha na kumuwezesha kupata mkate wake wa kila siku.

Safari ya mziki

Historia ya Ibraah

Ibraah alianza kuimba akiwa na miaka nane. Hapo alikuwa kidato Cha pili. Alipenda kuimba sana na kuzifuatilia nyimbo za wasanii waliokuwa juu wakati huo.

Siku moja baada ya kutoka shule, Ibraah alikuwa yuapita katikati ya soko huku akiimba nyimbo kama kawaida yake. Alikutana na mjombake Mabrouk nyoya anayejulikana kwa jina la utani kama duke boy. Vile alikuwa anaimba, Duke boy alipendezeshwa na kumshauri Ibraah kuanza kurekodi nyimbo zake huku akijitolea kusimamia gharama zote.

Baada ya mda, Ibraah alirekodi nyimbo zake kadhaa chini ya uongozi wa meneja wake duke boy.

Mwaka 2015, Duke boy aliamua kuingia kwa siasa kwani alikuwa mmoja wa waliogombea kiti Cha ubunge Cha Tandahimba constituency. Hii ilimsaidia Ibraah kwa safari yake ya mziki kwani alikuwa akizunguka na duke boy kwenye campaign tour zote.

Siku moja kulikuwa na mshindano ya kuimba huko mtwara na Ibraah alikuwa mmoja wa washindani. Mshindi alikuwa apate Tsh 100,00. Ibraah alishinda mashindano hayo na kupokea hiyo hela. Hii ilimuezesha Ibraah kuhudhuria tamasha zaidi za wasanii wakubwa Tanzania.

Kukutana kwa Ibraah na Harmonize

Safari ya Ibraah kukutana na harmonize iliaanza mwaka wa 2016. Duke boy alimuahidi Ibraah kwamba atafanya juu chini mpaka awakutanishe na Harmonize. Ibraah alitamani sana kukutana na harmonize kwani alijua angepata nafasi nzuri ya kuwa mmoja wa wasanii wa konde music worldwide.

Ibraah alifanya bidii sana ili aweze kukutana na harmonize. Mwaka wa 2017 aliamua kufanyia biashara zake dar es salaam ili iwe rahisi kwake. Akiwa huko, Ibraah alipokea simu kutoka kwa duke boy akimjulisha kwamba, harmonize alikuwa na tamasha maeneo ya Masasi. Bila kupoteza mda, Ibraah alijipanga kuelekea Masasi ili kupata nafasi kutumbuiza kwenye hilo tamasha. Alijua akifanya hivo itakuwa rahisi kwake kupatana na Harmonize. Kwa bahati mbaya, hiyo siku Ibraah hakuweza kuonana na Harmonize kwani harmonize alikuwa na shughuli nyingi.

Ibraah hakufa moyo na kila Mara harmonize alikuwa kwa tamasha, Ibraah alikuwa akihakikisha kwamba ana kuwa mmoja wa wasanii wenye ku perform ili angalau aweze kukutana na harmonize ila haikuwa rahisi.

Kwa bahati nzuri, duke boy alizipata namba za simu za harmonize na kumpa Ibraah ili ajaribu kuwasiliana naye. Harmonize hakuwahi kupokea simu ya Ibraah hata siku moja. Labda Harmonize hangeweza kupokea simu kwa mtu ambaye hamjui ni nani.

Mwaka wa 2019, safari ya Ibraah ya mziki ilianza mkondo mpya. Duke boy alipata kazi ya udereva na kuwa dereva wa mamake harmonize. Hii ilikuwa rahisi kwake kupatana na Harmonize na siku moja alimpigia simu Ibraah akitaka aje studio ya harmonize, “Sinza studio”. Ibraah hakupoteza wakati na alifika kwa mda. Huko alikutana na producer bonga pamoja na beauty Mmari ambaye ndiye meneja wa harmonize.

Wawili hawa walimuomba Ibraah kuimba mbele yao ili waweze kufahamu uwezo wake. Walipomusikiza Ibraah, walimuomba aende zake nyumbani na watampigia simu baadae.

Baada ya siku tano, Duke boy alimpigia simu Ibraah ili aje arekodi nyimbo kwa producer bonga ili waweze kumpatia harmonize hiyo nyimbo aisikize. Baada ya siku kadhaa, Ibraah alipata simu kutoka kwa harmonize akitakiwa kukutana naye.

mpenzi wa Ibraah

Hii siku ilikuwa kubwa sana kwa Ibraah na alionekana mwenye Raha sana kwani aliona ndoto zake zikitimia. Harmonize alimuomba harmonize aimbe mbele yake na baadae kumuamuru awe akija ofisini kila siku ili kusaidia kazi za ofisi na pia kurekodi nyimbo. Baada ya mda, Ibraah alisajiriwa na konde music worldwide

Mwaka wa 2020, Ibraah alirekodi nyimbo yake ya kwanza “Nimekubali” chini ya label ya Konde music. Nyimbo hii ilikuwa kubwa zaidi Tanzania na wengi wakamfahamu Ibraah zaidi. Baada ya mda aliachia Ep yake ya kwanza kwa jina ” Steps” iliyokuwa na nyimbo tano.

Nyingi za nyimbo kwenye hiyo Ep zilikuwa ni kolabo na wasanii wakubwa kama vile Joe boy na skiibii. Baadae aliweza kufanya Kazi mpya na harmonize iliyojulikana kama one night stand

Nyimbo za Ibraah

  1. Nani
  2. Subira feat Skiibii
  3. Wawa Feat JoeBoy
  4. Njiwa
  5. Wandoto
  6. One Night Stand Feat Harmonize
  7. Nimekubali
  8. sawa
  9. My Queen
  10. Nitachelewa
  11. Magufuli
  12. Hayakuhusu

Mpenzi wa Ibraah

Kulitokea fununu kwamba Ibraah walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ibraah baada ya Nana kuonyesha tattoo yake ya shingo yenye jina ya Ibraah. Ibraah alipoulizwa kama yeye na nana ni wapenzi alikataa na kusema yeye bado ni single boy. Nana naye hajawahi sema chochote kuhusiana na hiyo tattoo.

Kama utakuwa haumufahamu Nana, ni video vixen aliyetumika kwa video ya Rayvanny iliyojulikana kama “I love you”. Kumbuka video hii ilizua gumzo na wengi wanasema ndio ilikuwa sababu kubwa ya fahyvanny kuachana na Rayvanny.

Utajiri wa Ibraah.

Ibraah anasemekana kuwa na nyumba ya kifahari na gari. Kwa sasa hatuna habari sahihi kuhusiana na utajiri wa Ibraah ila inasemekana utajiri wa Ibraah ni kama $200,000.

Hiyo ndiyo historia ya Ibraah natumai umefahamu Mengi kuhusiana na msanii huyu wa konde Gang. Zidi kutegea na kufuatilia habari zetu za hapa mwangaza news ili uweze kutafahamu mengi zaidi.

Soma hii pia: historia ya Harmonize

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *