AfyaMaisha

Fredie Blom kutoka afrika kusini amesherehekea miaka 116

Fredie Blom kutoka afrika kusini amesherehekea siku yake ya kuzaliwa leo. Ni miaka Mia moja tangu dadake auliwe na homa “Spain flu” lakini yeye ako na bahati kwani amesherehekea miaka 116.

“Nimeishi miaka mingi kwa uwezo wa mwenyezi Mungu kwani pia sio rahisi kwangu Mimi kuwa mgonjwa,” hayo ni maneno yake Blom anayesemekana ndiye mzee sana ulimwengu mzima.

Fredie Blom birthday

Wakati akihojiwa, Fredie Blom alisema anakumba nwaka wa 1918 ambapo watu zaidi ya milioni kumi waliaga dunia dadake akiwa mmoja wao.

Blom alizaliwa mwaka wa 1904 sehemu inayojulikana Kama Adelaide ilioko mlimani winterberg nchini afrika kusini.

Blom anasemekana ni miaka mingi kuliko raia wa uingereza aliyetajwa Kama mzee katika Guinness book of record. Mzee huyo wa uingereza alisemekana kuwa na miaka zaidi ya miaka 112.

Miaka ya Blom haiendani na mwili wake kwani anaonekana mwenye afya zaidi. Wakati wa kusherehekea kuzaliwa kwake, wajukuu wake walionekana wenye furaha na majirani pia walijitokeza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa

Fredie Blom kwa maisha yake amekuwa mkulima ndani ya Capetown. Alikutana na mke wake Jeanette ambaye ana umri wa miaka 86 kwenye club na baada ya kucheza naye, uhusiano wao ukaanza hapo.

Fredie Blom na mkewe Jeanette

Wawili hawa wamekuwa kwa uhusiano kwa miaka 30 na kwa Sasa wako Capetown. Blom alisema hatakubali Coronavirus imtie hofu

Fredie Blom ni mzee anayependa sugars sana na ako na hofu kwa uhaba wa sigara nchini afrika kusini kwani kwake zawadi kubwa siku ya kuzaliwa kwake ni sigara.

Fredie Blom anasema Mara ya mwisho kumuona daktari ilikuwa miaka miwili iliyopita. Blom hakufanikiwa watoto Ila anaishi na wanawe wa Jeanette aliowazaa na mme wake wa kwanza.
Watoto hawa humpenda sana japo sio babayo wa kweli.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *