Sanaa

Kutana naye mwelekezi/director wa tamthilia ya Pete

Najua unamfahamu nimimi, nuru, jasiri, sudi, Mbura na waigizaji wengi Ila ukiulizwa mwelekezi/director wa tamthilia ya Pete, utakosa jibu.

Tamthilia ya Pete ni sinema inayopeperushwa kila siku ya wiki katika maisha magic plus. Pia tamthilia hiyo hupeperushwa siku ya jumatatu mpaka jumatano ndani ya maisha magic East. Ni wengi wanafahamu waigizaji Ila walio nyuma ya pazia hawajulikani kwa sana.

Tamthilia ya Pete imetayarishwa na Daudi Anguka ambaye amezaliwa hapa pwani japo nyumbani kabisa ni upande wa kisumu. Sinema hii kwa Sasa imepata umaarufu sana na huenda ikawa kubwa zaidi kwani kila unayekutana naye anaipatia sifa za kumwaga.

Janet Chumbe ni mmoja wa timu inayotayarisha Tamthilia ya Pete. Yeye ni mwelekezi na hii sio kazi yake ya kwanza. Janet aliwahi kuwa mwelekezi wa sinema ya kalimani dynasty iliyokuwa ikipeperushwa ndani ya KTN. Kulingana na wanaomfahamu zaidi, Janet ni mwelekezi mwenye hapendi mchezo akiwa kazini. Kama unataka kuelewana na mwelekezi huyu wa tamthilia ya Pete, Basi fanya Kulingana na maagizo yake.

janet director wa tamthilia ya

Janet Chumbe amechangia sana kuboresha kwa tamthilia hii maana wengi wanaoigiza pale wamejifunza mengi kutoka kwake. Kama wewe ni mvivu kazini basi huwezi kufanya kazi na janet. Mwelekezi huyu huhakikisha mda uliowekwa umetumika vipasavyo na Kama wewe sio mtu wa kurauka utapoteza kazi.

Janet mwelekezi ama director wa tamthilia ya pete
Janet Chumbe akiwa kazini

Janet hafanyi kazi hii peke yake. Kunaye mwelekezi mkuu ambaye ni Sharif, Sharif ni mwelekezi mkuu katika tamthilia ya Pete. Ni kijana mpole sana lakini anafahamu mengi sana kuhusiana na filamu. Akili yake hufanya kazi kwa haraka sana na hajawahi lemewa na kazi yake. Tuseme kwamba, Janet chumbe amejifunza zaidi kutoka kwa mwelekezi huyu

sharif director wa tamthilia ya pete
Sharif Mohammed aliyevaa shati ya rangi ya samawati

Tamthilia ya Pete hutayarishwa na timu ya watu wengi na hii ndio sababu kuu ya ubora wake. Daudi Anguka amehakikisha wafanyi kazi wake wanaelewa filamu na wamehitimu kwa njia moja au nyengine.

Kwa Leo tunakomea hapo. Endelea kufuatilia habari zetu za mwangaza news kwa mengi zaidi. Usisahau ku subscribe kwa kubofya kengele nyekundu ilioko pale chini pembeni upande wa kulia.

Soma hii pia ( Sanaa ya pwani kwa undani zaidi)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *