MzikiSanaa

Wasanii wa Mombasa kwa undani zaidi | Tatizo Nini?

Ni wengi sana hawawezi kuwataja majina wasanii wa Mombasa. Sanaa ya pwani ni mojawapo ya sekta inayosemekana kutengwa kwa mda mrefu. Kuna wasanii wa Mombasa waliojaribu bahati yao na kwa wengi bidii yao imezaa patupu. Kulingana na washikadau, Kuna wivu ndani ya Sanaa ya pwani na kila aliyefanikiwa huogopa sana kushiriki na mwenzake.

Baadhi ya wasanii wa mombasa wamekuwa wakilaumu uchawi kwa baadhi ya wasanii, Ila hakuna aliye na ushahidi kuhusiana na wasanii wanaotumia nguvu za uchawi. Ili uweze kufaulu ndani ya eneo la pwani, mpaka uwe na bidii ya mchwa maana hata uwe na kipaji haimanishi utakuwa kwenye kilele.

Sio wanamziki tu, ma DJs pia Wana matatizo yao pia. Unaweza ukamkia bonge la status kwa mitandao kutoka kwa baadhi ya ma DJs wakilaumiana. Dili nyingi sanasana za county huzua taharuki na Mara nyingi anayejulikana ndiye hufaidi, wazungu wanasema connection.

Wengi  wamejitokeza kujaribu kuunganisha wasanii wa Mombasa lakini mwishowe mambo hugeuka na bidii Kama hii hukosa kuzaa matunda. Ni hivi juzi John chacha alijaribu kuwaunganisha wasanii wa eneo la pwani Ila mwisho wake ikawa ni matusi kwenye whtsapp group na wengi kujitoa wakidai Kuna upendeleo.

Wasanii wa Mombasa wamejitenga wengi wao wakitengeneza makundi yenye kwangu Mimi hayana Nia njema. Ukitaka kujua Kama wasanii wamejitenga vikundi, tazama msanii anapoachia nyimbo. Ni watu wake wa karibu watakao ongelea kuhusu kazi yake mpya na kuisambaza kwenye mitandao lakini wengine wataitazama tu huku wakitafuta vile wataikosoa.

Mambo Kama haya yanapelekea wasanii wengine kuvunjika moyo na kuacha mziki kabisa maana hawapati nafasi kwao na Sanaa ya pwani kubakia kwa wachache. Cha kuvunja moyo Ni kwamba mpaka watangazaji wa radio eneo la pwani pia wamegawanyika. Ili wacheze mziki wako kikamilifu lazima waweze kunufaika na jasho lako.

Kuna wasanii wako chini ya usisimamizi wa watangazaji wa redio na hii limechangia pakubwa sana kudidimia kwa Sanaa ya pwani. Gavana wa county ya Mombasa amekuwa mstari wa mbele kuweza kuwasaidia wasanii wa pwani na Kama unafuatilia kila sherehe za county lazima utapata wasanii wa Mombasa njia inayotumika kuchafua wasanii hao siijui na sitoweza kuongelea kwa sasa.

Wasanii wengi waliozaliwa hapa pwani huhamia Nairobi ili waweze kupata usaindizi kwani wanaamini ndani ya jiji kuu Kuna namna ya kupenya. Kadhaa wamefaulu Ila wengi wamefeli.

Masauti ni mmoja wa wasanii waliofaulu baada ya kuhamia Nairobi. Haikuwa rahisi kwake kwani Mara ya kwanza alipochukuliwa na teddy Josiah,mambo hayakufunguka alivyotarajia. Kulingana na utafiti wangu, teddy Josiah ni Kama hakumuelewa msanii maana alimlazimisha kufanya mziki uliopitwa na wakati huku akidai siku moja watu wataelewa. Naona watu walikataa kuelewa kabisa na sio masauti tu, iddi singer pia ashawahi kufanya mziki kwa teddy Josiah mambo yakawa yaleyale.

Wacha niachane na story za teddy Josiah maana leo naongelea Sanaa ya pwani. Je, wamkumbuka Bably Omar?. Alikuwa producer ndani ya tabasam record na kusema kweli Kama Kuna producer aliweza kuisukuma Sanaa ya pwani Basi sio mwingine Ila Ni Bably omar. Kwa bahati mbaya producer huyu aliweza kusafiri marekani na kuiacha Sanaa ya pwani kwenye mdomo wa mamba.

Wakati wote Sanaa ya pwani inapotajwa, Kuna baadhi ya watu lazima watajwe. Wako katika makundi tofauti Kama vile wasanii, DJs, watangazaji, producers na wengine wengi.

Susumila

Susumila na Mbosso - wasanii wa Mombasa
Susumila na Mbosso

Ni msanii anayesemekana kuwa na bidii sana. Anajulikana sana sio hapa pwani tu Ila Kenya nzima na afrika mashariki kwa jumla.

Ameweza kufanya kolabo na wasanii wakubwa Kama vile Mbosso, lavalava, king kaka, na wasanii wengi tajika. Kama Kuna msanii anaogopewa zaidi na wasanii wa eneo la pwani ni susumila.

Wengi wao hudai susumila huhusika na mziki unaopeperushwa ndani ya radio nyingi za pwani. Wengi wanasema ana uwezo wa kumshawishi mtangazaji wa radio asicheze mziki wako.

Sio hayo tu, wengi husema susumila ni mganga na alipofikia ametumia nguvu za giza. Sijui ni kwa Nini wasanii humuogopa sana na msanii mwenyewe anaonekana mpole na Hana maneno na watu. Mpaka Leo nyimbo yake sonana aliyomshirikisha Mbosso inafanya vizuri.

Susumila na gavana wa mombasa Ali Hassan Joho ni Kama mtu na kakake. Susumila huingia kwa gavana Joho mda wowote anapojisikia. Inasemekana wawili Hawa wamekuwa marafiki hata kabla ya Joho kuwa mbunge wa kisauni.

Susumila yuko na Bibi na watoto. Bibi yake Anajulikana Kama Ruth. Kumbuka aliwahi kumwacha Ruth kwa mda na kumuoa kibibi. Baada ya kuzaa mtoto mmoja na kibibi waliachana na akarudi kwa mke wake wa kwanza ambaye ni Ruth. Haikueleweka haya yote yalifanyika vipi maana ni Kama miujiza Ila wacha nikomee hapo maana sijui la ziada.

Susumila ni msanii Kati ya wale wasanii wakongwe anayefanya vizuri ndani ya Sanaa ya pwani akilinganishwa na wengine wengi. Ana meneja zaidi ya wanne akiwemo Gates mgenge kutoka pwani f.m na Chris wa milele f.m.

Nyota Ndogo

Nyota ndogo | Sanaa ya pwani
Nyota ndogo | Sanaa ya pwani

Kuna mengi kuhusu msanii huyu wa kike Ila nitajaribu kugusia machache. Kulingana na historia yake, nyota ndogo alikuwa msaidizi wa kazi za nyumbani kabla hajaanza usanii. Talanta yake ilijitokeza na producer kutoka ujerumani aliyejulikana Kama madebe aliweza kutambua talanta yake na kuamua kumsaidia.

Wakati nyota anaanza mziki, hakukua na ushindani mkubwa Kama Sasa na hii ilichangia sana kujukikana kwa haraka. Nyimbo zake hupendwa zaidi kwani Zina mafunzo chungu nzima. Wasanii kutoka nchi jirani ya Tanzania wanamfahamu kabisa msanii huyu wa kike. Ashafanya kolabo na wasanii kadhaa wa Tanzania akiwemo Mr. Blue na lady Jay dee.

Nyimbo yake iliyomuweka kileleni ni “watu na Viatu”. Wamama wanampenda sana kwani mwanadada huyu hana majivuno. Amesaidia wengi sana na pia anawalisha wengi. Amesaidia wamama kujenga nyumba za kukodisha na jinsi ya kujitegemea kimaisha.

Kwa Sasa ameolewa na mzungu na Kama unakumbuka vizuri alikuwa kwenye uhusiano na Kshot ambaye ni producer Ila waliachana kwa sababu ambazo hatuzijui.

Ally B

Ally B
Ally B

Anajiita rais wa ziki la Nazi. Ni msanii ambaye ni vigumu kumkosa katika tamasha za kimataifa. Kama Kuna msanii amefaidi katika sherehe za kimataifa Basi ni Ally B. Alikuwa mmoja wa wasanii waliochaguliwa kusaidia kwenye campaign ya jubilee.

Kwenye stage huacha wengi midomo wazi kwani anaelewa wafuasi wake wanachokipenda. Hana maringo na roho yake Safi imechangia pakubwa mno kufaulu kwake.

Juzi aliweza kufanya kolabo na Masauti na kusema kweli nyimbo hii aliifanyia haki. Ana uwezo wa kufanya style Aina nyingi zikiwemo za kitamaduni.

Amoury

Amoury na Producer Shirko
Amoury na Producer Shirko

Ni msanii wa katikati ya mkoa wa pwani ama ukipenda mvita. Amekuwa kwa game kwa mda Sasa na Kama amekuwa ukifuatilia Sanaa ya pwani, alikuwa mmoja wa kikundi Cha Sav Clan.

Na rafiki yake wa karibu wa mbunge wa mvita mheshimiwa abdulswamad na chochote kuhusiana na usanii, abdulswamad humfikiria amoury kwanza. Amoury na susumila ni wasanii wanaosemekana kuwa haziendi. Nikisema hivo namaanisha kuwa wawili hao hutofautiana kwa maswala mengi ikizingatiwa wote wanajuana na wanasiasa tajika wa mkoa wa pwani.

Amoury aliwahi kufanya kazi na producer Totti wakati producer Shirko alikuwa yuko nchini Tanzania. Producer Shirko aliwahi kuwa mmoja wa sav clan kabla hajasafiri Tanzania na baada ya kufanya kazi Tanzania kwa mda wa miaka kadhaa, producer Shirko aliamua kurudi Kenya japo kwa Sasa kikundi Chao Cha Sav clan hakipo Tena.

Dogo Richie.

Dogo Richie
Dogo Richie

Ni msanii aliyetokea jungle master’s yenye ilikuwa ikiongozwa na prince adio na producer Emmy d. Ana kipaji na ni mwandishi mkubwa. Sio mchoyo wa kufanya kolabo na wasanii wa chini maana amesaidia wengi “japo kwa malipo”. Kuandika nyimbo kwake ni Kama biashara na Kama una sauti Ila kutunga nyimbo sio mambo yako, Basi ndogo Richie atakusaidia.

Hupenda sana kuongea wazi na Mara nyingi msanii huyu huamua kurekodi nyimbo na kuwataja wanao haribu Sanaa ya pwani bila kuogopa mtu yeyote. Ni juzi tu aliweza kurekodi nyimbo na kumtaja gavana wa mombasa Ali Hassan Joho na kudai anapenda ku support wasanii wa nje kuliko wasanii wa pwani.

Anasemekana kuwa na uhusiano wa kifamilia na Willy m tuva ambaye ni mtangazaji katika radio citizen. Wengi husema ndogo Richie ndiye aliyechukua nafasi ya Sudi boy ambaye kwa Sasa yupo Nairobi.

Chikuzee.

Chikuzee
Chikuzee

Ni msanii hatari, kama orodha ya wasanii wa Mombasa inatajwa, Basi chikuzee lazima awepo, ako na sauti ya kipekee na kwa kweli yeye ni kiungo muhimu katika Sanaa ya pwani. Chikuzee aliweza kufanya colabo kadhaa na susumila japo wawili hao walikuja kukosana.

Alikuwa chini ya musa babaz ambaye ni kakake chief kiumbe Ila kwa Sasa hawako pamoja tena. Kwake usanii ni biashara na Kama una Nia ya kumtumia, umenoa maana badala ya yeye kufanya kazi ya bure, afadhali abaki kwake nyumbani.

Kaalamoto

Kaalamoto
Kaalamoto

Ni msanii wa michano. Ni mkali sana katika mtindo huru na anaweza akaongelea chochote bila kunakili.

Juzi aliweza kufanikiwa sana baada ya kuiuza album yake nakala nyingi zaidi kushinda wasanii wengi hapa pwani. Msanii huyu anafaa kumshukuru sana Gates mgenge kwani alichangia sana katika utambulisho wake.

Aliwahi ku host kipindi ndani ya pwani Tv Cha Wana hip-hop kabla ya tv station kufungwa. Mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuwa ameoa Ila kwa Sasa sijui Kama bado yuko kwenye uhusiano.

Jovial

Jovial
Jovial

Ni msanii mwenye sauti ya kutoa nyoka pangoni. Ana kipaji na wengi wanampenda. Alishawahi kufanya kazi na Otile Brown Ila kwa sababu ambazo hatuzijui, wawili hawa waliacha kufanya kazi pamoja.

Otile Brown aliweza kumnunulia Gari jovial akamuonyesha na kumruhusu apige picha nayo alafu akampokonya. Na juzi tu jovial alijitokeza na kusema Otile Brown hakuwahi kumnunulia Gari na inaonekana ilikuwa kiki wasemavyo wa bongo.

Jovial ni mmoja wa wasanii waliohamia Nairobi, wazungu husema “kutafuta green pasture”. Kwa Sasa bado yupo Nairobi

Twenty 2

Twenty 2
Twenty 2

Ni msanii mpole sana na wengi humsahau. Ana bidii kwa kazi yake tuseme tu mda bado haujafika Ila anapoamini ni kuwa one atakuja kuweka historia.

Habari za hapa na pale zasema msanii huyu anapokea usaidizi kwa Anna mpenzi na Salim mapapa ambao wanaishi ujerumani. Wawili Hawa humsaidia twenty 2 kwa kazi zake za kisanii Kama vile kusimamia utayarishaji wa video zake na mengine mengi.

Twenty 2 ameoa na ana watoto wawili. Huwa hana haraka na usanii na huenda Ana kazi nyengine mbali na usanii.

Wasanii wengine wa mkoa wa pwani ni Kama vile

  1. Pday
  2. Alkenia love
  3. Cnew

 

Hao ni Kati ya wasanii tajika katika mkoa wa pwani. Siwezi kutaja wengi maana wako wengi na Wana uwezo mkubwa sana. Kati ya wasanii wapya wenye hawajakuwa kwenye Sanaa kwa mda ni pamoja na

  1. Ali mahaba
  2. Adasa
  3. Akeelah
  4. Sai Kenya

Kabla nimalizie, Kuna watu kadhaa ningependa pia kuwatambua kwani uwepo wao umeinua Sanaa ya pwani.

Gates mgenge.

Gates Mgenge
Gates Mgenge

Ni mtangazaji katika radio ya pwani FM. Alijiunga na pwani FM hivi maajuzi baada ya kutoka pilipili F.M. Kama unakumbuka vizuri gwiji huyu alikuwa pwani FM hata kabla ya kujiunga na pilipili. Aliweza kuinua wasanii wengi mmoja wao akiwa kalamoto.

Wasanii wengi walijulikana kupitia kwake. Ana vipaji vingi sana kwani pia yeye ni MC. Kama unapanga sherehe ama una zoezi flani unahitaji MC Basi Gates mgenge ni mmoja wa wale MC hatari.

John chacha

John Chacha | The Don

Anajulikana kwa jina maarufu Kama the don. Hujitolea sana ili kuisaidia Sanaa ya pwani. Hutumia hata hela zake za mfukoni bila kujali Kama zitarudi au la.

Anapenda mziki wa pwani na anajivunia kuwa mmoja wa Sanaa hii. Mara nyingi husafiri Hadi Nairobi na hela yake ili kuutangaza mziki wa pwani.

Amewahi kupanga tamasha nyingi hapa pwani ili kuinua Sanaa ya pwani. Hivi majuzi alichaguliwa Kama kinara wa Sanaa ya pwani.

Guy G

Nitakuwa nimekosea sana nikimalizia bila kumtaja huyu bwana. Wengi watakuwa hawamfahamu kwani yeye siye mwanamziki Ila ana husika pakubwa sana na Sanaa ya pwani.

Guy G ni mtayarishaji wa filamu na kusema kweli wasanii wengi wa mkoa wa pwani wamepitia mikononi mwake.

Katika miaka ya hapo nyuma aliweza kuwatambulisha wasanii wengi wa pwani akiwemo sudiboy, susumila,sav clan, na wengine wengi.

Sio wasanii wa pwani tu Ila gwiji huyu ashawahi kufanya kazi na Alikiba, doggman, matonya na wengine wengi. Mpaka leo bado anazidi kutayarisha video za wasanii japo kidogo nasikia fununu hapatikani kwa sana kwani siku hizi ni mmoja wa watarishaji wa tamthilia ya Pete yenye hupeperushwa mnet. Pia anatayarisha nyanya rukia ambayo pia ipo Maishamagic Mnet.

Kwa leo nitakomea hapo na nakuomba uzidi kufuatilia habari zetu za mwangaza news kwa mengi zaidi. Pia unaweza subscribe kwa kubofya kengele nyekundu ilioko pale chini upande wa kulia.

Video mpya ya Avril

Soma hii pia (Niko tayari kuolewa Tena : Bety kyalo )

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *