Mchipuko

Wakristo nchini ujerumani waruhusu waisilamu kufanyia ibada kanisani

Wakristo nchini ujerumani wamewaruhusu waisilamu kufanyia ibada kanisani kutokana na kukosa nafasi katika msikiti wa Dar Assalam

Mnamo tarehe nne mwezi wa tano, ujerumani iliruhusu nyumba za ibada kufunguliwa lakini Sheria zifuatwe za kuachana kwa nafasi ya 1.5m Kati yao.

Imekuwa vigumu kwa msikiti wa Dar Assalam ulioko Neuk├Âlln district kuweza kutoshea waisilamu wote maana sio mkubwa sana ikizingatiwa Sheria za kuachana kwa nafasi ya 1.5m

Kanisa ya the Martha Lutheran church ilioko Kreuzberg ilijitokeza na kuwapa nafasi ndani ya Kanisa hiyo waweze kutumia ili kufanyia maombi ya ijumaa. Hii ndio ilikuwa swala ya mwisho kwa waisilamu ya mwezi mtukufu wa Ramadan.

Mwezi wa ramadan huwa mhimu sana kwa waisilamu. Mwezi wa ramadan waisilamu hujieka karibu na mwenyezi Mungu na kusali zaidi. Katika mwezi huu waisilamu hufunga kula, kunywa kufanya na kufanya mapenzi kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Dar Assalam waisilamu wakiswali kanisani

Hii haikuwa kawaida nchini ujerumani na sio tu ujerumani mbali ulimwengu mzima kwa jumla. Katika mwezi wa ramadan, waisilamu hufanya maombi kwa pamoja Ila hii haikuwezekana mwaka huu kwani wengi walifanyia maombi manyumbani mwao.

“Mbali na kuleta madhara mengi, janga hili limeleta umoja na tunafaa tushukuru.. wakati mwingine majanga ndio huleta watu pamoja. Tunashukuru tulipata nafasi ya kufanyia Sala na Asante kwa waliojitolea..'” hao ndio yalikuwa maneno ya Imam.

“Mwanzo ilikuwa ni vigumu kufanyia maombi pale ukiangalia Kuna vyombo vya mziki, picha mbalimbali na vitu vingineo Ila tulisahau vitu hivi vyote na tukaweza kufanya maombi yetu maana hii ni nyumba ya Mungu pia.

Soma hii pia ( Uhuru aeleza vile uchumi wa kenya utakavyo fufuliwa)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *