Mziki

Azziad Nasenya ( Queen of Tiktok) pamoja na Ringtone waachia Nyimbo

Ni mwanadada anayezidi kugonga vichwa vya habari. Azziad Nasenya alipata umaarufu wakati alijirekodi akikata mauno nyimbo ya Femi One na Mejja ndani ya Tiktok. Tokea wakati huo amekuwa maarufu na kwa sasa wengi wanamfahamu.

Azziad Nasenya zoea kupigwa mawe

Azziad Nasenya ni mwanahabari na kutokana na umaaurufu alioupata, aliweza kujipatia kazi katika nyingi ikiwemo kazi moja ndani ya kituo cha televiseni. Azziad Nasenya ndiye alichangia pakubwa kwa kuisambaza nyimbo ya Utawezana ya Femi one na Mejja. Kulingana na femi one, Azziad Nasenya hakusaidia pakubwa sana kuipa umaarufu nyimbo ya Utawezana. Kulingana na femi one, Utawezana ilipata umaarufu hata kabla Azziad Nasenya hajajirekodi ndani ya Tiktok.

Azziad Nasenya Tiktok queen
Azziad Nasenya Tiktok queen na Ringtone

Ringtone ambaye ni msanii wa nyimbo za injili amechukua nafasi ya umaarufu wa queen of tiktok Azziad na kuweza kumtumia kwa video yake mpya- Zoea mawe. Kulingana na video ama nyimbo hii mpya, Ringtone anahimiza wale waliofanikiwa wazoee kufuatwa na maadui kwani mti mwenye matunda haukosi kupigwa mawe.

Azziad Nasenya amefanya kazi nzuri kwa hiyo video na kusema kweli hii video inamfaa yeye kwani amepitia mengi sana baada ya kupata umaarufu wake.

Soma hii pia ( Utawezana yake femi one na mejja yazidi kupaa)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *