Mchipuko

Harmonize atangaza kufungua kituo Cha Radio na Tv

Ripoti tunazoipokea kwa sasa ni kwamba ” Harmonize atangaza kufungua kituo Cha Radio na Tv”

Harmonize ambaye Jina lake kamili ni Rajabu Abdul kahali ameamua kufuata nyayo za diamond platnumz na kwa sasa anataka kuanzisha kituo Cha radio kama alivyofanya mwenzake diamond.

Harmonize child

Harmonize kwenye page yake ya Instagram alitangaza hayo huku akiongeza kwamba baada ya radio pia ataanzisha kituo Cha runinga hivi karibuni.

Hiki ndicho alichokiandika kwenye Instagram stories

“Kondegang FM and Kondegang TV 100% tonight. God is good,”….

Harmonize alipata umarufu na kujulikana zaidi baada ya kufanya Kazi na wasafi label japo baadae aliamua kutoka kwenye label ya wasafi inayoongozwa na diamond platnumz na kuanzisha label ya Konde Gang.

harmonize photos

Alipotoka kwenye label ya wasafi, wawili hao, diamond na harmonize walianza ugomvi mpaka sasa inaonekana label ya wasafi na konde Gang ndio wanaopeana ushindani mkubwa kwa sasa nchini Tanzania.

Ni hivi majuzi tu harmonize alitangaza kwamba amechoka kuishi peke yake na yuko tayari kutafuta mchumba atayemuoa. Kumbuka ni kama mwezi mmoja umepita baada ya harmonize kuachana na kajala.

Harmonize atangaza kufungua kituo Cha Radio na Tv

Harmonize ambaye ni Mkurugenzi wa Konde Gang hupenda sana kuweka wazi akiwa na uhusiano na yeyote yule. Ndio maana juzi aliandika kwa ukurasa wake wa Instagram kwamba japo anaishi maisha mazuri, Kuna kitu kinamfanya ajihisi hajakamilika. Kulingana na yeye, akipata mke hapo ndipo maisha yake itakuwa imekamilika kabisa.

mtoto wa harmonize

Kwa sasa harmonize ako na watoto wawili na ameahidi kwamba mwanamke atakaye pata kwa sasa atafanya ndoa naye na wazae watoto.

” Najua maisha yangu ni mazuri, Nina starehe za kila aina, nyumba yangu ni kubwa na yenye gharama lakini natamani kuwa na mwanamke.. nitampenda maisha yangu yote.. nimechoka kuwa mpweke Sikuumbwa kuchezea wasichana…! And my next love story lazima itafika kwenye ndo na watoto,” Harmonize aliandika haya…”

Mwanamke wa mwisho harmonize kuwa naye ni kajala na uhusiano wao uligonga mwamba wakati harmonize alisemekana kumtongoza Paula ambaye ni mtoto wake kajala. Kwa sasa Paula anasemekana kuwa mpenzi wa Rayvanny na wawili hawa wametangaza kufunga ndoa Paula atakapo maliza masomo yake.

Kabla ya harmonize kuwa na kajala, alikuwa na Sarah Michelloti mwanamitindo kutoka Italia. Waliachana na mpaka sasa inasemekana bado wanaishgulikia talaka yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *