Maisha

Mapenzi: “Usimuite daktari ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho”

Mapenzi ni kitu mhimu sana kwa wawili wanaopendana. Haijalisha mumeishi pamoja kwa mda gani. Mapenzi yanaweza ikakufanya uwe chizi ama ukajitoa uhai na hiyo yote ni kwa sababu unampenda mtu flani.

Ajuza mmoja alikuwa yuagua na bwanake alipoona kwamba huenda akafariki aliamua kumuita daktari ili aweze kumshughulikia mke wake. Mke wake alimkataza kwani alijua mwisho wake ulikuwa tayari ushafika.  Alimuita bwanake na kumwambia maneno haya.

Usimuite daktari, nataka nilale salama huku nikiwa kwa mikono yako. Sitaki kupata matibabu maana siku yangu imeshafika na naona ni wakati wangu wa kukuaga…..

Ajuza huyu alimkumbusha bwanake mapenzi yao ya zamani na vile wawili hawa walikutana. Ilikuwa raha kwa wawili hawa japo ilikuwa siku yao ya mwisho kuwa pamoja hapa duniani. Wawili hawa walipigana busu na chaajabu ni kwamba badala ya kulia, wote walikuwa wakitabasamu kwa furaha.

Nakupenda sana mume wangu na nitazidi kukupenda kwa dhati, naye bwanake akayarudia yake maneno vilevile….

Baada ya maneno hayo yule ajuza alifunga macho na kupumzika kwa amani. Mume wake hakulia kwani alijua wazi kwamba ameachwa salama na hakuwa na la kufanya Ila kukubali matokeo.

Kila mtu hapa duniani huja  mkono mtupu isipokuwa mapenzi tu na pia anapotoka hutoka bila chochote Ila mapenzi tu.  Pesa tulizonazo kwenye Benki, Kazi ama ajira yetu, nyumba, mashamba ni vifaa tu vya kutuwezesha kuishi vizuri.

Tunafaa kupendana sana hapa duniani kiasi kwamba ni kama hatuna lingine la kufanya hapa duniani. Kumbuka baada ya hapa Kuna maisha mengine na utaulizwa maswali ya ulichokifanya hapa duniani. Kumpenda mwenzako hakuna gharama yeyote ile na kama kakukosea yeyote yule unafaa kumsamehe ili naye mwenyezi Mungu aweze kukusamehe makosa yako.

Kumbuka mwenyezi Mungu katika vitabu vyake takatifu anatuhimiza tuwe watu wa kumsameheana kwani yeye pia hutusamehe. Mpende mwenzake kwa Moyo wako wote, awe mpenzi ama jirani. Kumbuka jirani wako atakuja kukufaa wakati mwingine na ataangalia matendo yako ya hapo awali.

Kwa Leo nakomea hapo, najua umejifunza kitu mhimu sana hapa na ningependa uweze ku share ujumbe huu na wenzako walioko Facebook, WhatsApp, Twitter ama popote pale. Huenda nao wakasaidika na wakazidisha mapenzi. Kumbuka ukisambaza Jambo njema kwa mwenzako utazipata baraka zake mwenyezi Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *