MaishaMchipukoSanaa

Historia ya Bahati Kenya

Bahati Kenya ni msanii wa nyimbo za injili Ila kwa sasa anafanya nyimbo za secular. Majina kamili Anajulikana kama Kevin Kioko. Alizaliwa mwaka wa 1992.

Bahati Kenya ni msanii anayejulikana sana nchini kenya sanasana wakati alikuwa akifanya nyimbo za gospel. Mziki wake wa injili ulipenya sana nchini kenya na nchi jirani na wengi walimjua kupitia mziki wake wa injili.

bahati first wife Diana marua

Historia ya bahati ni kama ya mtoto mwingine yeyote aliyelelewa sehemu iliyokosa matumaini Ila mwenyewe ana ndoto za kufaulu maishani. Bahati ni yatima kwani mamake aliaga wakati akiwa shule ya chekechea. Babake mzazi alioa tena na kuhamia sehemu nyengine.

Bahati diana marua

Bahati na Babake hawakuwahi kukutana tena kwa mda wa miaka nane. Bahati aliteseka sana mpaka ikabidi ajiunge na kituo Cha watoto yatima kijulikanacho kama ABC children’s home maeneo ya Mathare.

Wakati akiwa kwa kituo Cha watoto yatima, bahati alianza kuvutiwa mziki. Alikuwa msemaji wa mashairi kanisani na shuleni. Mwaka wa 2010, bahati akiwakilisha shule ya St. Teresa’s Boys ilioko eastleigh kwenye mashindano ya mziki kiwango cha kimataifa iliyofanyika mjini Nakuru. Wakati huo alikuwa yuacheza guitar.

Historia ya Bahati Kenya

Mwaka wa 2013, safari yake ya Mziki ilichukua mkondo mpya baada ya kuachia nyimbo yake ya kwanza kwa jina “siku ya kwanza”. Kwenye hiyo nyimbo bahati aliongelea kuhusu siku yake ya kwanza ya kuokoka. Nyimbo hii ilipata kuchezwa sana kwenye radio.

bahati age : how old is bahati

Mwaka huo huo wa 2013, bahati alikuwa miongoni ya wenye walichaguliwa kuwania tuzo za groove awards. Hii sherehe ilihudhuliwa na rais wa Kenya mheshimiwa uhuru kenyatta na ilitangazwa mojamoja kwa runinga nyingi barani afrika na kupata utazamaji wa mamilioni ya watu.

“Wangu’ ndio nyimbo ya bahati iliyofuatia, nyimbo hii ilikuwa colabo na Mr Seed. Baadae aliachia ” Mama” iliyomfungulia njia zaidi. Baada ya Mama, bahati aliamua kuimba kuhusu maisha yake na hapo ndipo akaachia “Machozi”. Video ya Machozi ilifanyiwa Mathare sehemu ambayo bahati alikuwa anaishi.

Kwenye video inaonekana bahati akiwahadithia watu waliokuwa wakiishi nao Mathare kuhusu maisha yake. Kwa mwaka mmoja, bahati alishinda tuzo saba ikiwemo new artist – groove awards 2013, most promising artist-mwafaka awards 2013, Best male artists coast awards 2013 na zinginezo.

Kwa sasa yuajulikana dunia nzima na kampuni nyingi zilizoko afrika mashariki zinamtumia bahati kwa matangazo ya biashara. Tamasha ambazo amehudhulia ni pamoja na 2012 groove awards party iliyofanyika Nyayo stadium pamoja na peace concert iliyofanyika Nakuru.

Tazama hii – Bahati ft. Nadia – Pete

Bahati ameoa mke mrembo kwa jina Diana marua. Ako na watoto wawili mmoja na Diana na mwingine na mwanamke tofauti. Hivi majuzi ameachia Ep yake kwa jina fikra za bahati inayofanya vizuri sana kwenye soko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *