Maisha

Naivasha trending sababu ikiwa vijana wa Subaru #SubaruBoys

Kwa siku kadhaa, naivasha imekuwa ikigonga vyombo vya habari. #Naivashatrending ndio hash tag imekuwa ikishikilia nafasi ya kwanza kwenye Twitter nchini kenya. Naivasha ni mji ulioko Kenya maeneo ya bonde la ufa.

Mashindano ya the world Rally Championships (WRC) safari Rally imepangiwa kung’oa nanga June 24 mpaka June 27 mjini naivasha na county ya nakuru. Kati ya mashabiki walioko huko ni wamiliki wa Magari Aina ya Subaru. Wengi washafika na wengine wako njiani kuelekea huko. Barabara kadhaa zitafungwa

Naivasha trending sababu juu ukiwa vijana wa Subaru #SubaruBoys

Naivasha inajulikana na vivutio vingi vya watalii Ila leo imekuwa tofauti kwani kwa sasa imekuwa kivutio Cha vijana wa Subaru. Inasemekana kwamba wamiliki wa Magari Aina ya Subaru hupenda sana kuwapeleka wanawake wao wa kando kama mafichoni.

Wengi wa wanaume hawa huwa wameoa na huwaacha bibi zao huku wakiwadanganya Wana shughuli za kikazi. Wanaume hawa huchukua mipango ya kando na kusafiri nao hadi naivasha ili kuwatumia kimapenzi na baadae huwaachia hela.

Wakenya wamewakosoa vijana wa Subaru maarufu kama #subaru boys kwani wanaharibu ndoa zao. Radio nchini kenya zimekuwa zikiongelea tukio hili kila mmoja akikashifu Ila wengine wametumia nafasi hii kama kichekesho.

Soma hii : vera Sidika na Brown mauzo watangaza uja uzito

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *