MaishaSanaa

Vera Sidika na Brown mauzo watangaza uja uzito

Vera Sidika na Brown mauzo watangaza uja uzito: Mfanyi biashara almaarufu kama Vera sidika ako na uja mzito na hivi karibuni atapata mtoto wake wa kwanza. Kama umekuwa ukifuatilia, kwa sasa vera Sidika Ako kwenye ndoa na msanii maarufu anayejulikana kama brown mauzo. Kulingana na Vera Sidika, brown mauzo ndiye mwanaume ameweza kukaa naye kwa mda mrefu kuliko wanaume wengine wote.

Vera sidika alitatangaza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya ku post video huku akionyesha uja uzito na kupapasa tumbo lake lanaloonyesha uja uzito wake. Huenda ikawa uja uzito wake ni wa miezi zaidi ya sita.

“Mapya yaja hivi karibuni…nakupenda sana mume wangu brown mauzo…aliandika vera Sidika….”

Vera Sidika na Brown mauzo watangaza uja uzito

Mashabiki wake walionekana kuwa na furaha kwani hawakupoteza mda na walianza kuujaza ukurasa wa vera Sidika na jumbe za kumsifu na kumpongeza huku wengine wakimkaribisha kwa Chama za wazazi.

Wengine walionekana wakimkejeli kwani walitaka vera Sidika azae na mwanaume mweupe ndio waweze kupata mtoto mweupe.

” Unafaa uzae na mzungu ndio mtoto wako angalau awe mweupe kwani ukizaa na brown mauzo mtoto wenu atakuwa mweusi kama wazazi wenu ….”

Vera naye hakuchelewa kuwajibu mashabiki zake kwani alionekana kujitetea akisema kwamba pia watoto weusi ni wazuri na Wana haki ya kuzaliwa. Alishangaa ni kwa nini watu wanaongelea kuhusu mtoto wake kuwa mweusi huku akishangaa kwani watoto weusi hawana shida gani

Soma hii : mapya kuhusu kifo Cha Chris kirubiĀ 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *