HistoriaMaisha

Historia ya Haji Manara

Kama umekuwa ukiitafuta historia ya Haji Manara basi utaipata hapa mwangaza news.

Mashabiki wa Simba SC humuita Haji Manara ‘ De La Boss’. Haji Manara kwa mda sasa ameifanya klabu ya Red lions kuwa timu bora afrika mashariki japo hali yake kama mnavyojua ako na albinism. Hii ni hali inayoogopewa kwani Kuna kipindi ilisemekana watu wenye hali hii ni hitaji kubwa sana kwa waganga.

Haji Manara biography

Badala ya kukata tamaa, Haji Manara alitumia hali yake ya albinism na kuwa kielezo chema nchini Tanzania huku akionyesha kwamba hata uwe na hiyo hali waweza kuwa mhimu kwa jamii.

Toka zamani, Haji Manara anapenda sana mpira wa miguu ama ukipenda football. Kumbuka alizaliwa kwa familia ya wanamichezo. Babake kwa jina Sunday Manara aliiwezesha nchi yake kushinda tuzo 43. Haji naye alifuata nyayo za Babake na alianza kupenda mpira akiwa bado mdogo. Babake Haji Manara ambaye ni Sunday Manara alikuwa anachezea nchi za nje kama vile Austria, Netherlands na USA.

Haji manara umri

” Babangu alinifanya nipende mpira kwani kila Mara nilimuona akicheza na nikatamani kuwa kama yeye.. kila akisafiri nchi za kigeni tulikuwa twaenda naye na nashukuru nilizunguka nchi nyingi sana… Kwa sasa Nina uwezo mkubwa na Mimi nimchezaji mahiri japo Kuna mambo kiasi yenye sikuyatimiza…. “

Haji Manara akiwa mdogo mjini Dar es salaam, alipelekwa kwa shule ya kuwafundisha watu kucheza mpira Ila kwa hali yake ya albinism, Haji Manara alikataliwa

Nchini Tanzania iko na albino wengi sana kuliko nchi nyingine yote ulimwenguni. Serikali ya Tanzania inafanya bidii kuhakikisha wanahudumiwa kama wananchi wengine bila ubaguzi wa rangi. Serikali isipofanya hivo basi huenda nchi ya Tanzania ikawa sio salama kwa watu wenye hii hali. Hali hii inaletwa na ukosefu wa “pigment” kwa ngozi, nywele na macho. Wengi huamini albino ni watu waliolaaniwa.

Haji Manara wikipedia

Haji Manara alizaliwa kariakoo na amekuwa Mkuu wa mawasiliano katika timu ya Simba SC. Amepitia mengi akiwa mdogo kwa sababu ya hali yake Ila hayo yote yamempa nguvu. Wengi walishangazwa na uwezo wake wa kucheza mpira kwani walidhani albinos hawana uwezo huo. Haji Manara alicheza kwenye michuano tofauti Zanzibar na kuchaguliwa kama mmoja wa timu ya wachezaji wasio zidi umri wa miaka kumi na sita. Baada ya kumaliza shule, Haji Manara aliendelea na mambo na mpira

Pia alisomea utangazaji na ashawahi Fanya Kazi ya utangazaji katika radio kadhaa ikiwemo uhuru FM kama mtayarishi na mtangazaji wa habari za michezo na siasa. Haji Manara anaelewa sana mambo ya michezo na hii ilimfanya achaguliwe kama football match commentaries.

Alikuwa mtangazaji wa pili ndani ya Tanzania kufanya Kazi hii ya football commentator. Wa kwanza kufanya hii Kazi alifahamika kama Leakey Abdala. Haji alifanya commentaries kwa runinga na hata radio hata Kuna mda aliwahi tangaza mpira wa world cup, Africa cup of nations pamoja na English premier league.

Haji Manara education background

Haji Manara anaamini kwamba, yeye kufanya Kazi na Simba kumebadilisha wengi kwani wameelewa kwamba hata albino wanaweza wakafanya projects kubwa. Anachofanya sasa ni kuhakikisha Kuna umoja kwa kila mtanzania bila kujali hali yake.

Kwa sasa klabu ya Simba inasemekana kufanya vizuri kwenye mawasiliano na pia kwenye mitandao na Kulingana na Haji, club yake ndio inafanya vizuri afrika mashariki. Vyombo vya habari vya nje kama vile BBC humfuata yeye kama wanataka maelezo yoyote kuhusu football ndani ya Tanzania na afrika mashariki kwa jumla.

“..Nchini Tanzania tunapenda matani, tunaweza tukakuingilia kwenye swala la football lakini mwisho wa siku tunachukulia tu kama matani…… Nchi yetu Ina umoja japo mashabiki wengine wanapenda sana kutukana kwa mitandao lakini ya mitandao inabakia huko huko kwani mwisho wa siku tunasaidiana…..”

wazazi wake hawakuona vibaya Haji Manara kuwa Simba wakati Babake ako yanga. Kulingana na yeye, hii iliongeza mapenzi. Mashabiki wa Simba wanapenda sana Haji Manara na wanamuita boss. Anasema mapenzi ya mashabiki wake inafanya hata asiweze kuwapeleka watoto wake matembezi kwani kila mtu anataka piga picha nao Ila sioni ubaya wowote juu pia nawapenda mashabiki wangu.

Kwa sasa tutakomea hapo kuhusiana na Historia ya Haji Manara. Zidi kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news kwa mengi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *