HistoriaMaisha

Historia ya Flaqo Raz ( Otis)

Kama ilivyo kawaida yetu hapa mwangaza news, tunapenda kuwafahamisha mengi kuhusiana na watu maarufu. Leo tuaongelea kuhusu Historia ya Flaqo Raz ( Otis).

Flaqo Raz alizaliwa tarehe 25 December. Ana talanta nyingi kwa pamoja, yeye ni mwanamziki,mchekeshaji na pia ni anaandika script. Ni mchekeshaji wa kwanza Kenya kuigiza kama wahusika watano tofauti akiwa peke yake. Cha ajabu ni kwamba kwa kila mhusika, Flaqo Raz anaigiza vizuri.

Flaqo Raz alianza kuigiza kama mama Otis. Mama Otis ni mama ambaye hapendi mchezo. Ni wale wazazi wanajua sana. Chochote wanachokifanya hukiona Kiko sahihi na maumizi wanayoyachukua ndio yanafaa yaani akikwambia kitu hufai Kupingana naye.

Mhusika Mama Otis anamfanya Otis apitie maisha magumu kwani hana uhuru wa kujiamlia. Wahusika wengine ambao Flaqo Raz ameigiza ni kama, Akoth, ambaye ni dadake Otis,Bakari na pia kama Babake Otis.

Erastus Ayieko otieno age

Haya ndio maisha ya Flaqo Raz

Flaqo ni muigizaji, mcheza ngoma, mwandishi na mchekeshaji kama wengi wanavyomfahamu.

Majina kamili ya Otis | Flaqo Raz

Anajulikana kama Erastus Ayieko otieno na alizaliwa katika hospitali ya Agha Khan tarehe 25 December ( Christmas day)

Masomo ya Flaqo Raz

Alisomea katika shule ya msingi ya Xaverian primary school, shule inayosemekana kuwa ya zamani sana katika eneo hilo. Aliendelea na masomo yake ya upili katika shule ya St. Mary’s high school kabla ya kujiunga na Jaramogi oginga odinga university ambapo alipata shahada ya public health mwaka wa 2018.

Akiwa shule ya msingi, Flaqo Raz alikuwa Kati ya wale wanafunzi ambao hawapendi mchezo na masomo. Hakupenda yeyote kumharibia ndoto zake za kuwa mtu mhimu kwenye jamii. Wakati huo haungedhania kuwa angekuja kuwa mchekeshaji mkubwa nchini Kenya.

mama otis real names

Maisha ya Flaqo Raz kabla ya umarufu

Baada ya kumaliza shule ya upili, Flaqo aliamua kutoka kwa wazazi wake alipokuwa akiishi na kuamua kuishi peke yake kama njia ya kujitegemea. Alijaribu mziki lakini akakuta Sanaa ya mziki sio rahisi kama alivyofikiria na akaamua kuachana na mziki. Akiwa kwa Sanaa ya mziki, Flaqo alipenda mziki wa Aina ya R&B ama ukipenda mziki wa mahaba. August Alsina ndiye alikuwa msanii anayependa kuiga. Baada ya kuona kwamba mziki wake hauendi popote, Flaqo alifikiria kuanza vichekesho. Baada ya kufanya uchunguzi, Flaqo aliwajulia mashabiki wake chenye wanapenda zaidi na akaelewa kwamba, wakenya wanapenda kusikia ama kutazama vitu ambavyo viko katika maisha ya kila siku. Hapo ndipo akamua kufanya aina ya vichekesho tofauti na wanachokifanya wachekeshaji wenzake.

Safari ya Flaqo Raz ya umarufu.

Kabla hajakuwa maarufu, Flaqo alikutana na watu wengi sana maarufu Ila walikuwa wakimpuuzia na hapo ndipo akaamua kupigania kilicho chake kama yeye. Video iliyomfanya ajulikane zaidi ni ile akaigiza kama khaligraph Jones na pia kama Bahati. Hii video ilimuongezea Flaqo mashabiki wengi sana na pia kwenye Instagram page yake akaongeza wafuasi zaidi ya elfu kumi Kwa mda wa siku mbili.

Flaqo 411 real names

Flaqo Raz kama mchekeshaji

Baada ya kukubalika kwenye Sanaa ya uchekeshaji, Flaqo aliamua kubuni wahusika tofauti kama vile mama Otis, baba Otis, Bakari na Otis. Bakari ni mcheza ngoma na hao wengine hucheza kama vile familia ya waafrika huishi na vile wazazi huishi na watoto wao. Flaqo Raz anasema alichukua uhusika wa mama Otis kwa maisha aliyoyapitia na mamake mzazi. Kulingana na Flaqo, mamake mzazi hakutaka Flaqo afanye Kazi ya uchekeshaji.

Wakati akianza uchekeshaji, wengi walivyodhania ana wazimu baada ya kupakia video ya mama Otis kwenye mitandao. Flaqo ilibidi ajifundishe kutengeza video kupitia kwa mitandao kama vile YouTube. Baada ya video yake moja kusambaa, wengi walifikiria ana pesa nyingi na watu wake wa karibu walitaka kuganyiwa pesa wakidhania ashakuwa tajiri.

Hii ilimfanya hata asile kwenye kibanda kwani wengi walidhania mtu kama Flaqo ni tajiri na hafai kula chakula Cha mtaani. Pia  ilikuwa vigumu kutumia matatu za kawaida kwani wengi walidhania ana gari yake.

Hii ilimfanya kupitia wakati mgumu mpaka akaamua kuingia kwa google ili kuelewa kwa undani zaidi maisha ya wale watu walianza kama maskini alafu baadae wakawa tajiri ili aweze kujua kama wenzake walipitia maisha kama yake. Kuna mda aliamua kurudi kwao kisumu alipoona maisha ya Nairobi yanampa mtihani. Baada ya kukaa kisumu kwa mda, Flaqo aliamua kutoyaskiza maneno ya watu na kuamua kurudi Nairobi.

Baada ya kukaa kwa mda, Flaqo Raz alikuwa haelewi kwa nini yeye hapati dili za kampuni kama vile wachekeshaji wenzake na alikuwa karibu ataka kuachana na uchekeshaji. Siku moja alipokea simu kutoka kwa kwa Brenda Jones alimhimiza kutokata tamaa kwani siku yake ingefika. Kusema kweli maneno yake Brenda Jones yalimtia Moyo na kwa mda mdogo Flaqo Raz alianza kupokea simu za biashara. Alipata dili na kampuni kubwa kama vile Samsung na Airtel.

baba Otis real names

Kwa maneno machache, tunaweza sema Flaqo Raz ni mpole na mcheshi, hupenda sana kucheka hata wakati mwingine huchekeshwa na vichekesho vyake. Flaqo anawashauri wenzake wanaochipuka wazidi kufanya bidii na wasikate tamaa kwani siku moja ndoto zao zitakuwa za kweli.

Pia anawahimiza wenzake kutoka nje na kufuata kilicho Chao kwani kufaulu hakuji rahisi na hakuna yeyote anaweza kukupa chochote chenye dhamani bila kutarajia malipo.

Flaqo hupenda kuwafuatilia mashabiki wake na chenye wanaandika kwa comments. Hupitia comments za kila mtu na husikiza mawaidha yao. Kulingana na yeye, lazima apitie comments ama meseji zote maana zingine humuletea Kazi.

Leo hapa mwangaza tutakomea hapo kuhusiana na Historia ya Flaqo Raz ( Otis).  Zidi kutegea mengi zaidi kupitia tovuti yetu

Soma hii pia: historia ya bahati Kenya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *