Historia Ya Rose Muhando
Rose Mhando ni msanii wa muziki wa injili kutoka Tanzania. Alizaliwa mwaka 1976 Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro katika familia ya Kiislamu. Alikuwa akisoma Madrasa baada ya shule lakini alibadili dini na kuwa Mkristo baada ya kuona maono ya Yesu Kristo. Rose ni mama wa watoto watatu na anajulikana kama Malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki. Zidi kuwa nasi ili ujue zaidi maisha na Historia Ya Rose Muhando
Maisha ya Rose Muhando
Alipokuwa na umri wa miaka tisa, alipatwa na ugonjwa usiojulikana uliomfanya alale kitandani kwa miaka mitatu. Alipona baada ya kuona maono ya Yesu Kristo. Rose Mhando ni mama wa watoto watatu. Alianza kazi yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya katika Kanisa la Anglikana la Chimuli mjini Dodoma. Baadaye alianza kuimba nyimbo zake za injili na akawa msanii maarufu na mshindi wa tuzo mbalimbali
Nyimbo Za Rose Muhando
Rose Mhando ana nyimbo nyingi za injili ambazo zimepata umaarufu na kupendwa na watu wengi. Nyimbo yake ya juzi ambayo imekuwa gumzo kote afrika yajulikana Kama Secret Agenda. Baadhi ya nyimbo zake ni:
- Waache Waende
- Secret Agenda
- Kama Mbaya Mbaya
- Wanyamazishe
- Yesu Karibu Kwangu
- Nibebe
- Ndivyo Ulivyo
Familia Ya Rose Muhando
Rose Muhando ni mama wa watoto watatu. Hata hivyo, haijulikani kama ana mume au la. Kuna uvumi kwamba alikuwa na uhusiano na mchungaji wa Kenya, lakini hakuna uthibitisho
Nyimbo Ya Secret Agenda ya Rose Muhando
Secret Agenda ni nyimbo moja kati ya nyimbo kumi na mbili katika albamu mpya ya Rose Muhando iliyotolewa mwaka 2022. Nyimbo hiyo inahusu jinsi Mungu anavyowalinda watumishi wake kutokana na mipango mibaya ya maadui zao
Masomo na Safari ya Mziki
Haijulikani kama Rose Muhando alimaliza masomo yake au la. Hata hivyo, alianza kazi yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya katika Kanisa la Anglikana la Chimuli mjini Dodoma
Utajiri wa Rose Muhando
Utajiri wake unakadiriwa kuwa kati ya dola milioni 1 hadi 5. Rose Muhando ameshinda tuzo mbalimbali kama vile Skiza Ring Back Tone of the Year mwaka 2011 na Best Singer in Tanzania mwaka 2009
Ni hayo tu kwa sasa kuhusiana na Historia Ya Rose Muhando. Natumai umejifunza mengi. Zidi kufuatilia habari zetu hapa Mwangaza kwani tuna mengi zaidi ya kuwajuza na kama kawaida kabla ya kuwajuza chochote huwa tunafanya utafiti dhabiti
Pia soma, Historia ya Jay Melody