Maisha

Makabila ya Tanzania

Hii orodha ya makabila ya Tanzania inaweza kuwa na matatizo kwenye majina kadhaa, kwa sababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya lugha za Tanzania inayopatikana katika Ethnologue, pamoja na tovuti nyingine.
Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja tu, badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Juu ya hiyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa “kabila,” lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Uarabuni au Uhindi.

Makabila ya Tanzania

Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
Waakiek
Waarusha
Waassa
Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang’ati)
Wabembe
Wabena
Wabende
Wabondei
Wabungu (au Wawungu)
Waburunge
Wachagga
Wadatoga
Wadhaiso
Wadigo
Wadoe
Wafipa
Wagogo
Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
Wagweno
Waha
Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
Wahangaza
Wahaya
Wahehe
Waikizu
Waikoma
Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
Waisanzu
Wajiji
Wajita
Wakabwa
Wakaguru
Wakahe
Wakami
Wakara (pia wanaitwa Waregi)
Wakerewe
Wakimbu
Wakinga
Wakisankasa
Wakisi
Wakonongo
Wakuria
Wakutu
Wakw’adza
Wakwavi
Wakwaya
Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
Wakwifa
Walambya
Waluguru
Waluo
Wamaasai
Wamachinga
Wamagoma
Wamakonde
Wamakua (au Wamakhuwa)
Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
Wamalila
Wamambwe
Wamanda
Wamatengo
Wamatumbi
Wamaviha
Wambugwe
Wambunga
Wamosiro
Wampoto
Wamwanga
Wamwera
Wandali

Soma hii hapa ( Magufuli awaonya wanahabari)

Haya pia ni Makabila ya Tanzania

Wandamba
Wandendeule
Wandengereko
Wandonde
Wangasa
Wangindo
Wangoni
Wangulu
Wangurimi (au Wangoreme)
Wanilamba (au Wanyiramba)
Wanindi
Wanyakyusa
Wanyambo
Wanyamwanga
Wanyamwezi
Wanyanyembe
Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
Wanyiha
Wapangwa
Wapare (pia wanaitwa Wasu)
Wapimbwe
Wapogolo
Warangi (au Walangi)
Warufiji
Warungi
Warungu (au Walungu)
Warungwa
Warwa
Wasafwa
Wasagara
Wasandawe
Wasangu (Tanzania)
Wasegeju
Washambaa
Washubi
Wasizaki
Wasuba
Wasukuma
Wasumbwa
Waswahili
Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
Watongwe
Watumbuka
Wavidunda
Wavinza
Wawanda
Wawanji
Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
Wayao
Wazanaki
Wazaramo
Wazigula
Wazinza
Wazyoba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *