Afya

Sababu za kuumwa na kichwa na matibabu yake

Kuumwa na kichwa ni mojawapo ya ugonjwa maarufu katika sekta ya afya. Watu wengi huumwa na kichwa wakati mwingi sana kwa sababu tofauti.

Sababu zinazochangia kuumwa na kichwa

  •  Msongo wa mawazo
  • Mkazo ama stress
  • Wasiwasi ama depression
  • Magonjwa ya blood pressure na pia migraine.
  • Jeruhi
  • Hali ya anga
kuumwa na kichwa
Picha kwa hisani

Kuumwa na kichwa kunaweza tatiza maisha ya binadamu. Ukijua chanzo Cha kuumwa na kichwa husaidia sana kujua hatua ya matibabu atakayo yachukua daktari.

Kuumwa na kichwa huenda kukawa tofauti kwa kila mtu. Kuna watu huumwa na kichwa upande mmoja ama kichwa kizima. Kuna mtu anaweza sema yuaumwa upande wa mbele, kando ama nyuma.

Huenda ukawa unaumwa na kichwa kwa sababu ya magonjwa mengine na pia huenda kichwa kikauma bila sababu ya ugonjwa mwingine. Kunazo Aina mbili za kuumwa na kichwa

  • Primary headache
  • Secondary headache

Primary headache

Hii hutokana na muundo wa kichwa na pia shingo. Sababu zinazoleta Aina hii ya kuumwa na kichwa ni kama;

  • Shida kwenye ubongo
  • Mishipa ya damu
  • kuzoea kutumia dawa

Secondary headaches

Hii inaletwa na mambo mengine tofauti ama magonjwa mengine. Sababu za secondary headache ni kama vile;

  • Uja uzito
  • Ugonjwa wa stroke
  • Uvimbe kwa akili
  • Maambukizi tofauti ama infection

Hii Aina ya kuumwa na kichwa ni hatari sana na inafaa kuchukuliwa kwa makini na utafute ushauri wa daktari kabla mambo hajakuwa mabaya zaidi.

causes of migraine
Picha kwa hisani

Kichwa huenda kikauma kwa mda, kwa siku, mwezi ama miaka. Ili kuelewa zaidi tumeweza kueleza hapa chini kwa makini zaidi.

Kama kichwa chako kitauma siku chache alafu kitulie, basi hii hujulikana kwa kimombo kama Episodic. Mara nyingi ukitumia dawa za kutuliza maumivu ama ukapata usingizi wa mda huenda kikaacha kabisa. Wakati mwingine huenda kikauma kwa siku kadhaa.

Kuna wengine huumwa na kichwa siku zaidi ya siku kumi na tano mfululizo ama karibia miezi mitatu. Hii inajulikana kama chronic headache

Kunayo Aina ya kuumwa na kichwa inayojulikana kama kipandauso kwa kimombo inajulikana kama  migraine. Migraine ni hatari zaidi na huuma upande mmoja wa kichwa japo hubadilika kila Mara, Mara waumwa upande, nyuma ama mbele.

Wakati unapokuwa na migraine, huenda ukawa na matatizo ya kuona vizuri na hata ukasikia kutapika.
Migraine pia huletwa na utumiaji mbaya wa dawa na ndio maana tunasema huwa ni mhimu kufuata maagizo ya daktari kabla ya kutumia dawa yoyote.

Ukiwa na migraine huenda ukawa na

  • maumivu ya shingo
  • msongomano ndani ya pua,
  • kukosa usingizi kwa wengine.

Kuna aina nyengine inayojulikana kama cluster headache. Hii huenda ikachukua dakika kumi na tano ama masaa matatu na huenda ikaja Mara moja mpaka Mara nane kwa siku. Hii inaweza jirudia Kati ya wiki 4 mpaka wiki kumi na mbili alafu inapotea kabisa. Cluster headache huwa yajirudia mda uleule kila siku. Cluster headache huenda ikasumbua kwa mwaka.

Tofauti ya cluster headache na Aina zingine tofauti za kuumwa na kichwa ni kwamba;

  • Uchungu wake sio mwingi
  • Uchungu kwenye mzunguko wa macho.
  • Jicho kugeuka nyekundu
    Kutoa chozi
  • Kufungamana kwa pua
    Kutoa jasho

iko Kutibu kuumwa na kichwa kunazo njia kama vile Kutumia dawa za kupunguza maumivu zinazojulikana kama nonsteroidal anti inflammatory drugs. Kama ni migraine dawa tofauti hutumika Kulingana na Maelezo ya daktari. Kumbuka kutumia dawa visivyo pia huchangia kuumwa na kichwa kwa hivyo hakikisha daktari anahusika.

Kutibu kichwa pia unaweza tumia njia rahisi ukiwa kwako nyumbani.

unaweza ukatumia donge la maji ama maji moto.

uiekelee kwa kichwa kwenye sehemu unayohisi uchungu. Pia maji moto kiasi unaweza yatumia. Ikiwezekana jiwekelee kitambala kabla ya kutumia maji ya donge. Tiba zingine ni kama;

  • kupunguza mawazo kwa kutafuta Jambo la kufanya ili usiwaze sana.
  • Kula chakula kizuri na upate usingizi wa kutosha.
  • Hakikasha sehemu unayolala haina kelele, haina joto na pia usisale na mwangaza.
  • Fanya mazoezi ya mwili kwani inapunguza mawazo na kuchangia afya nzuri.
  • Punguza ukunywaji wa Pombe na unywe maji mengi.
  • Unapofanya kizi yoyote sanasana ya ofisini, jipe pumziko ili uweze kujinyosha na kupumzisha macho

Soma hii pia : faida za ulaji wa mabenda)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *