Afya

Njia za Kupunguza uzito

Kuna watu wengi sana wamekuwa wakiulizia jinsi ya kupunguza uzito ama ukipenda uzani. Kwa kawaida, kuongeza mwili huwa ni rahisi Ila kupunguza inaweza kukugharimu mda mrefu sana na wakati mwingine hata hela ndefu ikatumika.

Mara nyingi ukiwa na mwili mkubwa basi jua afya yako ipo hatarini na huenda ukapata magonjwa sugu kutokana na uzani wa mwili wako.

Kuna wazazi wengi huongeza mwili wakati wakiwa wajawazito. Hii ni kawaida kwa wengi. Wengi wa hawa wazazi huchukia sana kuwa katika hali hii ya unene na hutafuta njia tofauti za kupunguza mwili.

Kuna watu miili yao ni minene na sio sababu wanakula sana Bali ni uridhi wa familia. Sio lazima wawe wanawake kwani wanaume pia wako. Wengi hufikiria kufanya mazoezi peke yake kunaweza kukapunguza uzito. Mazoezi bila kula kwa mipangilio huchangia kuongeza uzito.

Ili kuweza kupunguza uzito lazima ule kwa mipangilio na kutotumia aina flani ya chakula. Ukiweza kuzingatia chakula na ufanye mazoezi, basi itakuwa rahisi kwako kupunguza uzito. Kumbuka pia mazoezi yataka mpangilio kwani waweza kuwa unafanya mazoezi yenye yaiwezi kuchangia kupunguza mwili.

Kama daktari wako amekushauri upunguze uzani lazima kuna njia sahihi ya kupunguza uzani.

Utafiti unaonesha binadamu anaweza kupunguza paundi 1 au 2 kwa wiki. Ulaji usio na mpangilio unaweza kukufanya kuhisi njaa mara kwa mara na bila kutosheka.

Hizi ndizo, sababu kuu ambaza zinaleta uzembe katika ulaji bora ,ila sio kila chakula kina matokeo hayo. Vyakula venye kiwango kidogo cha carbohydrates vina punguza uzani na ni rahisi kuvipata

Hizi ni njia barabara za kupunguza mwili;

 • Kupunguza hamu ya kula kuna sababisha kupunguza uzito haraka
 • Kula chakula kenye madini ya sahihi.

NJIA TATU ZA KUPUNGUZA MWILI.

 • Punguza vyakula venye carbohydrates.

Njia rahisi ya kupunguza mwili kwa haraka unafaa kuachana na vyakula venye sukari na starches kama vile mihogo mchele na vinginevyo

Kwa kufanya hivo utapunguza hamu ya kula kila mara na kula vyakula venye kalori kidogo.

vyakula vya madini bora

chakula cha kupunguza uzito
Picha kwa hisani

Chakula chako kinapaswa kukuwa

 • protein
 • Mafuta
 • mboga

Na kiasi kidogo cha carbohydrates kama vile nafaka nzima(whole grains)

Protein inayotakikana kwa vyakula ni;

 • nyama
 • kuku
 • samaki
 • mayai

Usiogope kujaza sahani yako mboga kwani ni muhimu zinapeana virutubisho kwa mwili mfano wa aina zamboga ni kama

 • Broccoli
 • Spinachi
 • Nyanya (Tomato)
 • Sukumawiki
 • Cabbage
 • Lettuce
 • Cucumber

Habari muhimu za afya;

Mwili wa binadamu unahitaji mafuta katika chakula chochote utakacho pika. Olive oil na parachichi ni chaguo bora katika chakula chako. Mafuta mengine kama siagi(butter) na mafuta ya nazi yakue kwa kiasi kidogo

zoezi.

Zoezi ni kitu muhimu katika mili yetu. kufanya zoezi mara tatu au nne kwa wiki kutakupa matokea kwa haraka kwa mfano kuendesha baiskeli kuruka kamba na kukimbia. Hizo ni baadhi za zoezi unapaswa kujitahidi kufanya kwa ajili ya afya njema.

Ukunywaji wa maji

Kama tunavyojua maji ni uhai maji yakinywewa kwa nidhamu na ukizingatia uzito mtu aliokuwa nao tunaweza kukwepa asilimia 60 ya maradhi mbalimbali.

mda gani sahihi wa kunywa maji?

 1. Mara tu unapoamka asubuhi
 2. Nusu saa au dakika 45 kabla ya chakula cha mchana au jioni
 3. Yanywe maji ukiwa umekaa kidogo kidogo
 4. Unaweza pia kuweka vipande vyalimau kwenye maji ili kuyapea ladha.

Kufikia hapo najua umejifunza njia nyingi za kupunguza uzito. Kumbuka katika njia zote nilizozitaja, lazima uwe na nidhamu kwani ni lazima ufuatilie njia hizi bila kukosa. Jaribu sana kuacha tabia ya kutamani chakula aina flani kwani huenda chakula hicho kikachangia kuongezeka kwa uzani wako.

Kama nilivyosema hapo awali. Kula kwa mpangilio na kufanya zoezi kunachangia afya nzuri ya mwili wako. Wakati unakula vizuri utaepukana na kumtembelea daktari kila Mara na kwa kufanya hizo utaweza kupunguza gharama ya maisha.

Tungependa uweze kuchangia na uweze kutueleza kwa comment hapa chini chochote ungependa hapa mwangaza news. Inaweza kuwa inahusiana na maisha ama afya. Asante sana kwa kuchagua mwangaza news.

Soma hii pia : sababu za kuumwa na kichwa na matibabu yake

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *