Nandy ft. Koffi Olomide – Leo Leo video
Nandy ft. Koffi Olomide – Leo Leo video
Baada ya kungojea siku mingi, hatimaye video ya Nandy ft. Koffi Olomide – Leo Leo imeachiliwa rasmi.
Ni juzi tu mashabiki wa Nandy walitaka kujua nini inaendelea kwani hiyo video imechukua mda sana kabla ya kuachiliwa. Nandy alimjibu shabiki mmoja kuwa footage imefutika. Hivi leo tumepata ukweli kwamba sio kama alivyosema Nandy kwani video ya Leo leo yake Nandy akimshirikisha koffi Olomide ipo hewani.
Ni hivi majuzi Nandy alijitetea iliposemekana anafuata nyayo za wasafi kwani diamond platnumz alipoachia kolabo na koffi Olomide naye Nandy alionekana kufuata nyayo za diamond. Nandy alisema yeye ndiye alikuwa wa kwanza kurekodi na koffi Olomide na kuja kwake tanzania juzi ilikuwa ni maswala ya kutayarisha video.
Kwa Mara ya kwanza hapa mwangaza, tazama Nandy ft. Koffi Olomide – Leo Leo video
Soma hii pia ( Nandy aeleza maisha yake na Billnass)