Sanaa

Majina kamili ya waigizaji wa selina maisha magic

Majina kamili ya waigizaji wa selina maisha magic

Kama wewe ni shabiki wa maisha magic na maisha magic plus, basi utakuwa ushaitazama Selina. Kama pia utakuwa mtu wa kufuatilia mitandao basi utakuwa umekutana na video aliyojirekodi tokodi alipokutana na rais Uhuru kenyatta na kumwambia “ona selina,, ona selina maisha magic…”

Ni tamthilia inayotazamwa sana hapa nchini kenya. Mashabiki wa tamthilia ya selina wamezidi kuongezeka kila kuchao. Bali na kuwa imeandikwa kwa ustadi, selina pia hupokea sifa chemchem na kusema kweli tamthilia hii hupokelewa vizuri.

Waigizaji wa selina maisha magic wanajua sana kuigiza na labda ndio maana selina inapata utazamaji mkubwa. Hadithi ya selina ni kuhusu msichana aliyezaliwa kwenye familia maskini na baada ya kupita mtihani wa kidato Cha nne, alitakiwa kujiunga na chuo kikuu. Mamake wakambo kwa jina Kristina hataki selina ajiunge na chuo kikuu. Anaamua kumuuza kwa familia ya mackenzie kama mfanyikazi hivo kutatiza kuendeleza masomo yake.

Je, selina ni tukio la kweli?

Wengi hujiuliza, je selina ni hadithi ya ukweli, hii ni kwa sababu matukio mengi yanayofanyika pale hutokea kwa maisha ya watu wengi. Waigizaji nao wanafanya hii tamthilia iwe tamu zaidi kwani kama ni hisia wanazijulia sana na wakati mwingine unaweza ukasahau kama unatazama uigizaji ukaona kama ni kweli. Kulingana na mwandishi, selina ni hadithi tu ya kubuni ila sio ya ukweli.

Selina ilianza na kumtambulisha muigizaji mkuu kwa jina Nelson. Nelson ni kijana anayetokea kwenye familia yenye pesa nyingi. Selina naye anafanya Kazi ndani ya hiyo familia. Familia ya Nelson inamiliki shamba la maua linayojukikana kama marembo flower farm.

Majina kamili ya waigizaji wa selina maisha magic

Pascallino Lpesinoi Lenguro Tokodi

Pascal tokodi selina maisha magic

Alizaliwa April 21, 1993 na kulelewa Rongai, county ya kajiado. Alianza kuigiza mwaka wa 2012 ndani ya kipindi Cha makutano Junction iliyokuwa ikipeperushwa ndani ya citizen Tv. Pia aliwahi kuigiza ndani ya Groove theory mwaka wa 2013 na pray & prey pamoja na Wrath zilizopeperushwa mwaka wa 2015 ndani ya Fox Africa na zinginezo.

Tokodi anacheza kama nelson lakini bali na yeye kuwa tajari, hajali kuwa karibu na mfanyi kazi wa nyumbani ambaye ni selina. Baadae anakuwa mpenzi wake selina.

Celestine Gachuhi

Celestine Gachuhi selina maisha magic

Ana umri wa miaka 25, ni mwanamitindo, mwanamziki na muigizaji hatari sana. Alianza kuigiza akiwa shuleni kwenye drama festivals na baadae akaanza kuigiza set books kwa stegi. Kulingana na tamthilia ya selina, selina amelelewa na mama wa kambo. Ni Kati ya wale waigizaji wakuu akiwa pamoja na nelson.

Peter Kamau

peter Kamau Biko Selina maisha magic

Alizaliwa sehemu moja maeneo kiambu na amelelewa na Babu yake na nyanyake. Alianza kuigiza zamani kidogo ndani ya national theatre na pia alijihushisha na uigizaji wa setbooks. Kwenye selina anacheza kama Biko. Huwa ni mpizani wa nelson kwani pia yeye anapigania penzi la selina. Aliwahi kuigiza kwenye Tahidi high iliyokuwa ikipeperushwa ndani ya citizen Tv.

Brenda Wairimu

Brenda wairimu Rossette selina

Japo kwa sasa hayupo tena, Brenda wairimu aliwahi kuigiza ndani ya selina. Alikuwa akishirikiana na Biko ili kuharibu mapenzi Kati ya selina na nelson. Katika selina, Brenda wairimu aliigiza kama Rossette. Nia yake ilikuwa selina na nelson waachane ili nelson awe mpenziwe lakini haikuwezekana kwani aliishia jela baada ya kutaka kumuangamiza selina.

Victoria Wakio Mzenge

Victoria Wakio Mzenge Kristina selina

Anaigiza kama mamake selina. Jina yake kwa tamthilia ya selina Anajulikana kama Kristina. Alianza kuigiza akiwa shule ya St. Augustine preparatory school. Victoria aliwahi kufanya kazi ya kanisa na alipojiunga na chuo kikuu aliendelea kuigiza. Alianza kuigiza rasmi mwaka wa 2014 na akaigiza ndani ya tamthilia ya pendo alipocheza kama Maria.

Abel Amunga

Abel Amunga Luke selina

Ni actor anayejulikana na wengi sana kwani pia huigiza kwa matangazo ya biashara ( adverts). Ameigiza kwenye filamu nyingi nchini kenya. Filamu hizo ni Kama senses 8, Taking the Flak, na zinginezo. Kwenye tamthilia ya selina anaigiza kama Luke.

Mbeki Mwalimu

Beki mwalimu husband age zoe selina

Mbeki anaigiza kama Zoe. Ni muigizaji mwenye uwezo mkubwa kwani alianza kuigiza zamani katika runinga na Theatre. Ameolewa na Regan ambaye ni kakake nelson Kulingana na hii tamthilia.

Irene Kamau

Irene Kamau pamela selina

Anaigiza kama dadake selina. Katika tamthilia ya selina Anajulikana kama pamela.

Helen Keli

Helen Keli patricia McKenzie selina

Anaigiza kama patricia McKenzie. Yeye ndiye mamake nelson. Anaigiza kama anayejali familia yake na anataka maendeleo kwa watoto wake bila mapendeleo.

Soma hii pia ( waigizaji wa maria citizen Tv)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *