Maisha

Mwanamke amuua mwanawe kwa kumchinja

Nchini kenya, Huzuni ilitanda katika Kijiji kimoja Cha Ndhiwa baada ya mwanamke kumchinja mwanawe shingo kwa kile alichokitaja kama mwanawe kukataa kunyonya.

Mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 23 anasemekana kumuua mwanawe Briton Ochieng’ huko Kijiji Cha Ng’ope, kata ya Konyango usiku wa jumamosi.

Tukio hili likitokea mda wa saa tatu usiku baada ya mtoto kuendelea kulia kwa mda huko akionekana kumsumbua mamake. Mamake aliamua kumnyonyesha ili anyamaze lakini badala ya kunyamaza aliendelea kulia.

Alimuweka chini na kwenda kuchukua upanga wenye makali na aliporudi alimrusha mtoto kwenye sakafu. Mtoto alipoendelea kulia, mama huyu alichukua upanga na kumkata nao shingo. Wanakijiji walipofika eneo hilo walimfunga mikono na kupeleka ripoti kwa naibu wa chifu, Gabriel Nyatame.

Kwa bahati nzuri Nyatame alimuokoa mama huyo kwa mikono ya wanakijiji waliokuwa na hasira kwani walitaka kumchoma kwa kile kitendo alichofanyia mwanawe.

“Nilifika kwenye eneo la tukio nikakuta tayari mtoto amekataa shingo, wanakijiji walimfunga mamake kwa kamba huku wakitaka kumchoma”, alisema Nyatame.

Mamake mtoto alikubali makosa yake na kusema aliyafanya yale baada ya mwanawe kukataa kunyonya.

” Hatujui ni kwa nini huyu mama amechukua hii hatua ya kumuua mwanawe lakini bado anasisitiza kwamba mtoto alikataa kunyonya ndio maana akaamua kumchinja.”, Nyatame alisema

Wakati wa tokeo hilo, Babake mtoto hakuwa. Mama mtoto alifikishwa kwenye kituo Cha polisi Cha Ndhiwa.

Robert Aboki ambaye ni polisi kwenye hicho kituo alisema ashamfungia mwanamke huyo na atafikishwa kotini haraka iwezekanavyo. Mwili wa mtoto yule umehifadhiwa katika chumba Cha watu Cha Manyatta Nursing home kilichoko kobodo trading center

Soma hii pia ( mazishi ya kiisilamu)

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *