MaishaSanaa

Wanainchi wampa makavu Pascal Tokodi a.k.a Nelson wa Selina maisha magic kwa kushindwa kujieleza kwa rais Uhuru kenyatta

Wanainchi wampa makavu Pascal Tokodi a.k.a Nelson wa Selina maisha magic kwa kushindwa kujieleza kwa rais Uhuru kenyatta.

  • Pascal Tokodi ni muigizaji wa tamthilia ya Selina maisha magic
  • Juzi alipata nafasi ya kuongea na rais wa kenya Uhuru kenyatta na kuipoteza nafasi hiyo
  • Wengi wamtetea Pascal Tokodi kwa kutoonyesha kumtegemea rais.
  • Badala ya kuomba usaidizi, Pascal Tokodi A.k.a nelson wa Selina maisha magic alimuomba rais Uhuru kuitazama Selina ndani ya maisha magic

Ni tukio ambalo limegonga vichwa vya habari. Juzi muigizaji mashuhuri wa tamthilia ya Selina, Nelson alipatana na rais Uhuru kenyatta katika pilka pilka zake za hapa na pale. Badala ya kumuomba msaada rais Uhuru kenyatta, Pascal Tokodi alitumia nafasi hiyo kutangaza tamthilia ya Selina huku akimuomba rais kutazama tamthilia hiyo ndani ya maisha magic.

Wengi hawakufurahia alichofanya Tokodi. Kulingana na wakenya wengi, Tokodi angeitumia ile nafasi kujitetea kama msanii na wasanii wenzake kwa jumla. Sio rahisi kupata nafasi kama ile na rais wa nchi kwani Mara nyingi rasi huwa yupo kwenye shughuli nyingi.

Kunao baadhi ya watu walimtetea Tokodi huku wakisema alichokifanya Tokodi ni Cha maana sana kwani alimuonyesha rais Uhuru kenyatta kuwa sio lazima apate msaada wa pesa ilhali ana Kazi yake na anajitegemea. Waliomtetea walidai ya kuwa sio lazima ukipatana na rais uanze kuomba msaada wa pesa, wakati mwingine muonyeshe kwamba unaweza jitegemea. Je wewe ungepatana na rais Uhuru kenyatta, ungemwambia nini? Tupia jibu lako hapo chini kwenye comments.

Asenteni kwa kuchagua mwangaza news, kama kawaida yetu tutazidi kukupa taarifa zinazogonga vichwa vya habari.

Soma hii pia ( Lavalava afunguka mazito anayoyapitia ndani ya wasafi label)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *