SanaaMchipuko

Lavalava afunguka mazito anayoyapitia ndani la label ya WCB

Lavalava afunguka mazito anayoyapitia ndani la label ya WCB

  • Lavalava amedai views zake zashuka kwenye youtube
  • Amesema yeye ni msanii mkubwa na anaweza akakaa mwaka bila kuachia nyimbo na bado akabaki juu
  • Lavalava ameomba mafans wake wazidi kumpa sapoti kwani siku moja mambo yatajipa.
  • Wakiwa wasanii zaidi ya wanne kwenye label ya WCB ni vigumu kila mtu apate nafasi sawa.

Kama unafikiria kuwa wasafi label vitu vinaenda vyenyewe, Basi utakuwa umekosea. Hii inadhihirika wazi kwa msanii lavalava ndani ya wasafi label. Kulingana na utafiti wetu Lavalava ndiye msanii anayeonekana kubakia nyuma. Ni juzi tu zuchu aliingia wasafi label na kwa sasa mziki wake umepenya ulimwengu mzima. Tazama msanii kama vile Rayvann, anajulikana zaidi na nyimbo zake zinapata views nyingi sana ndani ya youtube. Mbosso mwenye alijiunga na wasafi majuzi pia yeye ako juu sana maana akiachia nyimbo, baada ya mda mfupi views zake hufikisha mamilioni. Je, lavalava ana tatizo gani?

Kulingana na mahojiano aliyowahi kufanya na Bongo 5, Lavalava alidai kuwa ni vigumu sana kila msanii awe juu kwa label moja kama wasanii wako zaidi ya wawili. Alipeana mfano ya watoto kwenye familia. Mzazi akiwa na watoto kadhaa, lazima utaona kama kuna mapendeleo kwa mtoto flani kwenye familia.

Lavalava anajiamini na yeye anajichukulia kama dhahabu na anaamini ipo siku moja atang’aa. Kuna taarifa iliyojitokeza kuwa wasanii waliopo wasafi wanamuona gere Zuchu kwani anaonekana kama anapendelewa zaidi. Lavalava alipoulizwa kama ni mmoja wa wale wasanii wanaomuonea wivu alijitetea na kusema hana hiyo roho.

Lavalava anasema husoma comments za mashabiki wake na wakati mwingine husononeka kwani wanaona kama hana bidii. Kulingana na yeye mambo kama haya humtesa sana akili ila anamuomba mungu kila siku ili amuepushe na hayo mawazo. Pia lavalava anadai mamake humsaidia sana kwa mawazo maana kila Jambo linalomkera humueleza mamake.

Video yake ya ipekeche haikupanda views kama za wasanii wengine hapo wasafi label, aliweza kufuatilia Jambo hilo na anayehusika na tekinologia akafanya bidii ili kutatua shida hiyo na kumuomba Lavalava ame mtulivu kwani hata kuna nyimbo za diamond platnumz zenye hushuka views pia.

Kwa sasa lavalava ameachia Ep “promise” ikiwa na nyimbo kama vile

  1. Wale wale
  2. Anaringa ft. Mbosso
  3. Komesha
  4. Far away ft. Diamond platnumz

Far away Lavalava ft. Diamond platnumz

Anaringa lavalava ft. Mbosso

Wale wale – lavalava

 

 

 

 

 

Soma hii pia ( Rayvann na Paula kajala yazua utata)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *