MchipukoMaisha

Video ya Rayvann na Paula yazidi kuleta utata huku kajala na hamisa wakijibizana

Video ya Rayvann na Paula yazidi kuleta utata huku kajala na hamisa wakijibizana.

kama umekuwa ukifuatilia mitandao basi utakuwa umekutana na habari kuhusiana na video ya kimahaba ya mtoto wa kajala ambaye ni paula na Rayvann. Ni video ambayo imezua gumzo kwani Kulingana na umri wa paula, haruhusiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi maana bado yuko shule.

Lawama zimerushwa hapa na pale kila mmoja akilaumu mwenzake kwa Jambo lililotokea. Kulingana na kajala, hamisa Mobetto ndiye wakulaumiwa maana ndiye aliyetoka na mwanawe Paula. Kajala anadai hamisa alipotoka na mwanawe Paula, alimpa pombe na kumkutanisha na Rayvann na hapo ndipo wawili hawa wakafanya video za kimapenzi.

paula Rayvann video

Hamisa Mobetto naye amejitetea vikali huku akitishia kumshtaki kajala. Hamisa ameeleza yaliyotokea na kabla ya kutoka na Paula alimpigia simu kajala ili amruhusu mtoto wake waweze kutoka naye. Baada ya chakula Cha mchana, hamisa Mobetto alimregesha paula nyumbani.

Hamisa ameweza kutetea jibu lake na kuweka picha zinazoonyesha utofauti wa nywele wakati yeye alikuwa na Paula na wakati paula anafanya video na Rayvann. Picha hizi zinazonyesha nywele ni tofauti kwa hivyo matukio haya mawili yalifanyika siku tofauti.

Paula ni mtoto wa kipekee wa kajala aliyemzaa na p. Frank majani yule producer aliyevuma sana enzo za hapo awali. Kwa sasa wawili Hawa hawapo pamoja na kajala anasemekana kuwa na uhusiano na Harmonize.

uhusiano wa harmonize na kajala

Harmonize naye hakuachwa nyuma kwa hilo swala la Rayvann na Paula kwani naye kwenye ukurasa wake wa Instagram aliweza kuweka ujumbe mrefu akimkemea Rayvann kwa kitendo alichokifanya. Harmonize aliomba serikali imchukulie hatua Rayvann kwani paula ni mtoto mdogo na kitendo alichofanya Rayvann kinafaa kuchukuliwa sheria.

Hapa mwangaza tunazidi kufuatilia hii habari na lolote likitokea tutakujuza kwani hamisa Mobetto na kajala huenda wakachukua hatua zaidi. Yetu jicho tu na kuwapasha habari. Zidi kutegea mwangazanews kwa habari za kuaminika na usisahau ku subscribe kwa kubonyeza kengele nyekundu iliopo pembeni ili uwe wa kwanza kupata habari zetu.

Soma hapa pia ( maisha ya Mbosso baada ya kuvunjika kwa yamoto band)

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *