MaishaMchipuko

Maisha ya Mbosso baada ya kuvunjika kwa yamoto band

Maisha ya Mbosso baada ya kuvunjika kwa yamoto band

Wakati mwingine huenda maisha yakakwendea mrama mpaka ukatamani kuiaga dunia. Haya yalimtokea Mbosso na akakata tamaa ya maisha yake na akaamua kuachana mziki. Kwa sasa, Mbosso ni msanii mkubwa sana ndani ya wasafi label inayomilikiwa na diamond platnumz. Kabla ya kujiunga na wasafi, Mbosso alikuwa yamoto band pamoja na wasanii kama vile Aslay na Beka flava.

Wakati yamoto band ilipovunjika, kila mtu alienda njia zake huku Aslay akiamua kufanya Kazi kivyake. Sio Aslay peke yake alifanya maamuzi hayo kwani akina Beka waliamua pia kufanya Kazi peke yao.

Mbosso hakuweza kuendelea na mziki kwani hela ilimpiga chenga na akaamua kurudi kijijini. Wakati msanii huyu yupo pale kijijini, alitamani sana kufanya mziki tena kwani wasanii wenzake waiokuwa nao yamoto band walionekana kufaulu hata baada ya kikundi chao kuvunjika. Maisha ya Mbosso ilichukua mkondo mpya na kwake ikawa vigumu kujikimu kimaisha. Kumbuka Mbosso alikuwa anategemewa na familia yake.

Akiongea ndani ya wasafi radio, Mbosso alieleza vile maisha yalikuwa magumu kwake ikizingatiwa ana mtoto nchini kenya aliyekuwa anamtegemea Mbosso kama Babake mzazi. Alikata tamaa kabisa na kuamua kujiunga na klabu ya mpira iliyoko humo kijijini kwao angalau aweze kuituliza akili yake.

Kwa bahati nzuri, Mbosso alikuwa ana uhusiano wa karibu na Rayvann. Rayvann a.k.a Vanny boy alimfaa sana Mbosso maana alimpa madili za kuandikia wasanii nyimbo na pia alikuwa alimsaidia na hela kidogo ya kujikimu kimaisha. Sio Rayvann tu aliyekuwa msaada kwa Mbosso bali rich Mavoko alimfaa Mbosso wakati huo mgumu. Wawili hawa walikuwa wakimtembelea Mbosso huku wakimpa moyo kuwa siku moja mambo yatakuwa sawa.

Mbosso aliwahi kumuandikia nyimbo queen darling ambaye ni dadake diamond platnumz. Nyimbo hiyo ilikuwa colabo yake queen darling na Harmonize. Jambo la kuchekesha ama kushangaza ni kwamba harmonize alimlipa Mbosso Elfu thelathini za tanzania. Mbosso hakuweza kukataa hiyo hela maana wakati huo alikuwa na mahitaji mengi na pia alihitaji tikiti aweze kurudi kijijini kwao.

Tokea huo mda, uhusiano wa Mbosso na queen darling ulichangia pakubwa sana Mbosso kupata nafasi wasafi. Mambo yake yalinyooka wakati alipigiwa simu na Mavoko ili wafanye colabo pamoja. Hakujua hiyo siku ndio atajiunga na label ya wasafi. Baada ya kufika wasafi, Mbosso alikutana na  meneja wa wasafi na kusajiliwa kwa label ya wasafi. Ndoto zake zilitimia maana alitaka sana kufanya Kazi na wasafi japo hakujua ataanzia wapi.

wasanii wa label ya wasafi

Kabla hajajiunga na wasafi, Mbosso aliwahi kupata jamaa kutoka sweden aliyejitolea kumsaidia baada ya mke wa yule bwana kuonekana kupendezwa na nyimbo za Mbosso. Mipango ya Mbosso na yule bwana kutoka sweden haikuweza kuzaa matunda kwani sio rahisi kupanga mambo ya kueleweka kama mnaishi nchi mbalimbali.

Soma hii pia ( wasanii tajiri afrika)

Mbosso anasema mpaka leo anaongea na yule bwana wa sweden maana hata kama mipango yao haikuingiliana bado alimsaidia sana kama kumlipia kodi wakati Mbosso hakuwa na hela.

Kwa sasa Mbosso ni msanii mkubwa sana ndani ya wasafi label. Nyimbo zake zimepenya dunia nzima na anapiga show za hela nyingi sana. Mbosso ana magari za kifahari na pia nyumba yake ni ya hela nyingi.

Mbosso anasema wasafi ni nyumbani na diamond platnumz ni Kama Babake. Hii Ina maana yupo pale na hana  mpango wowote wa kuiaga label ya wasafi.

Maisha ya Mbosso inafaa kuwa funzo kwetu aidha wewe ni msanii ama mtu wa kawaida. Wakati unaona kama mwisho wako umefika, elewa kwamba kuna Mwenyezi Mungu ambaye anakutazama. Hawezi kubali uteseke kila siku. Kuteseka ni mtihani wa mda tu alafu baadae mambo yananyooka. Cha msingi ni kufanya bidii kwa chochote kile unachokifanya.

Kumbuka Mungu hawezi kukupa mtihani maisha yako yote. Elewa kwamba Mungu ni mwaminifu na ana mipango mizuri juu ya maisha yako. Zidi kutegea mwangazanews kwa habari za kuaminika. Usisahau ku subscribe kwa kubonyeza kengele nyekundu iliopo pembeni ili kila siku uwe wa kwanza kuzipata habari zetu zenye ukamilifu.

Tazama video yake Mbosso – Fall

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *