MchipukoMziki

Mbosso afunguka ni kwa nini hajafanya kolabo na diamond platnumz

Mbosso afunguka ni kwa nini hajafanya kolabo na diamond platnumz.

Kama umekuwa ukifuatilia mitandao na wewe ni mfuasi wa mziki wa Mbosso basi utakubaliana nami kuwa hajawahi fanya kolabo na boss wake ambaye ni diamond.

Karibia wasanii wote pale wasafi wamefanya kolabo na diamond platnumz ila mpaka wa leo, Mbosso bado hajawahi achia nyimbo yoyote na boss wake. Wengi hujiuliza ni kwa nini hili halijawahi fanyika ikizingatiwa kwamba Mbosso ni msanii hatari zaidi. Hivi majuzi, Mbosso aliweza kuelezea ndani ya wasafi radio mambo yote kuhusiana na tukio hilo.

Mbosso diamond platnumz

Mbosso alidai kwamba sio eti hajafanya Kazi na diamond platnumz, amefanya Kazi nyingi naye na zipo ndani ya studio huku wakingojea siku Maalum ya kuachia Kazi mojawapo ya hizo nyimbo.

Mbosso alisema kwa mda wa karibia siku tatu yeye na diamond wawekuwa studio wakichambua ni Kazi gani wataachia mwanzo ila bado hawajakubaliana ni Kazi gani inafaa itoke mwanzo.

Mbosso alisema anatamani sana ile siku ataweza kuachia kazi yake na boss wake diamond Platnumz kwani diamond ni msanii mkubwa duniani na kuachia nyimbo na yeye huenda ikapenya na ikasikizwa ulimwengu mzima kwani diamond Anajulikana zaidi duniani kuliko msanii yeyote afrika mashariki.

Zidi kutegea habari zetu hapa mwangaza news kwani kama kawaida tunaelimisha na pia tunawapasha habari kama zinavyo chipuka.

Soma hii pia ( maisha ya Mbosso baada ya kuvunjika kwa yamoto band)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *