Sanaa

Waigizaji wa huba maisha magic bongo

Waigizaji wa huba maisha magic bongo

  • Ni tamthilia inayopendwa zaidi nchini tanzania
  • Nandy ambaye ni msanii mkubwa wa kike tanzania anaigiza ndani ya Huba
  • Huba imetayarisha na Lulu Hassan ambaye ni mtangazaji nchini kenya

maisha magic bongo logo

Kusema kweli, kuanzishwa kwa chaneli ya maisha magic bongo kumeokoa vipaji vingi sana hapa Tanzania. Baada ya chaneli hii kuanzishwa, wengi wamepata ajira na kusema kweli inaleta burudani ya Hali ya juu kwa sinema nzuri kama vile Huba, sakafu, mizani ya ushambenga, harusi yetu na zinginezo.

Huba ni tamthilia ya kitanzania inayopeperushwa ndani ya maisha magic bongo. Inahusu familia mbili zenye hazina uwelewano mzuri kwani Kila familia inataka kuwa na nguvu za uongozi.

Kulingana na familia hizi, pesa kwao ndio Kila kitu na ndio maana hawawezi kuelewana maana Kila familia yataka kuonekana na pesa zaidi na kama unavyojua pesa huleta ubinafsi hivyo kuongeza matatizo ya kila siku.

Inafikia hatua mapenzi ndio pekee inayoeleza kuleta suluhu na kufaulu katika maisha ya familia hizi mbili lakini usisahau kwenye mapenzi hakukosi kukosana.

Ukilinganisha na chaneli zingine, maisha magic bongo Ina ubora wa Hali ya juu kwani picha yake na sauti zipo kiwango cha juu sana. Maisha magic bongo Ina watazamaji wengi sana nchini tanzania na nje ya nchi..

huba bongo movies actors actress

Tamthilia ya huba maisha magic iliaachiliwa mwaka wa 2017. Ikilinganishwa na tamthilia zingine, huba ndio tamthilia ambayo imedumu sana kwa Tv kwa miaka mingi na maaruufu sana kwani iko na watazamaji wengi mpaka wa nchi jirani Kenya.

Huba iko na waigizaji wanaochipuka na wakongwe ambao ni maaruufu kama vile, muhogo mchungu, fatuma makongoro, mboto haji, Abdul Ahmed a.k.a Ben Blanco  na wengine wengi

Nandy ambaye alikuwa msanii wa kwanza wa kike kupata 10 million views kwa youtube afrika mashariki na pia ni msanii maaruufu nchini Tanzania pia yupo ndani.

Kwa sasa Nandy ni main actress kwa tamthilia ya huba na anacheza kama mwanamke anayetafuta pendo baada ya kusalitiwa na mpenzi wake wa hapo awali.

Huba imetayarishwa na Lulu Hassan, tv presenter nchini kenya ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Jiffy Pictures. Kampuni ya Jiffy Pictures imetayarisha tamthilia zingine kama vile, Kovu, maza, Aziza na Moyo

Soma hii pia ( waigizaji wa Pete maisha magic)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *