InternationalMaishaSanaa

Nandy aeleza walivyokutana na Billnass

Nandy aeleza walivyokutana na Billnass

Kila mmoja ana historia ya walipokutana na mpenzi wake. Maajabu ya siku hizi ni kwamba kuna waliokutana kwenye mitandao na kwa sasa wamefunga ndoa, wamezaa watoto na kujenga familia pamoja.

Nandy na Billnass pia Wana historia yao. Kulingana na Nandy, wawili hawa walikutana kwenye tamasha. Vile Nandy alikuwa mgeni kwa mziki, Billnass alikuwa alimsaidia sana kwa mambo kadhaa kuhusiana na swala nzima la mziki.

Kabla ya hiyo tamasha, Billnass alipenda sana ku’like picha za Nandy kwenye instagram na hapo ndipo urafiki wao ulianzia. Kulingana na Nandy wawili Hawa walikuwa wanachat kabla hawajakutana.

Maisha ya Nandy na Billnass

uhusiano wa Nandy na Billnass

Nandy anasema wakati Billnass amekasirika, hurusha madongo labda kwa njia ya nyimbo ama maneno. Hii hutokea Kama Kosa alilofanya Nandy ni kubwa na kama ni kosa ndogo humuita Nandy ili waweze kuongea. Kwa upande wa Nandy Billnass akimkosea yeye hununa na huwa hataki kumuongelesha kabisa Billnass.

Inasemekana Nandy hapendi kukubali makosa yake na huwa ni mgumu sana kuomba msamaha. Billnass amesema amemfundisha Nandy kukubali makosa yake na kwa sasa sio kama hapo awali.

Billnass sio mgumu wa kuomba msamaha na akijua amemkosea Nandy basi hufanya bidii kumuomba msamaha kupitia sms ama kumfuata sehemu yeyote alipo kumuomba msamaha.

Kulingana na Nandy, Billnass anapenda sana simu na mda mwingi huwa yupo kwenye simu. Hupenda sana kuchat kwenye ma group ama kuskiza hotuba kwenye youtube. Nandy anasema amejaribu kumkomesha Billnass hiyo tabia lakini ameshindwa. Nandy naye anasemekana ni mtu wa wivu sana na kumuelekeza huwa kuna ugumu sana.

Soma hii ( je, kuna ugomvi Kati ya Nandy na zuchu?

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *