HistoriaMchipukoSports

Historia ya Cristiano Ronaldo : Maisha ya Cristiano Ronaldo

Karibu tena katika tovuti yetu ya mwangaza news na Leo Nataka nikueleza mengi kuhusiana na Historia ya Cristiano Ronaldo. Najua unaweza kuwa unayafahamu machache kuhusu Gwiji huyu Ila kwa sasa nataka nikueleze mengi kuhusiana na maisha ya Cristiano Ronaldo, familia yake, safari yake kama mwanasoka na mengi zaidi.

Maelezo mafupi kuhusiana na historia ya Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro ni mchezaji kutoka nchi ya Portugal. Mwaka wa 2003 Cristiano Ronaldo akiwa na umri wa miaka 16, Manchester united walilipa £12 million ambazo ni zaidi ya $14 million za marekani ili kumsajili. Kwa pesa hii, Ronaldo aliweka rekodi kwa kulipwa pesa nyingi akiwa na umri mdogo.

Mwaka wa 2004 wakati wa ligi ya FA cup final, Ronaldo aliipatia Manchester united ushindi kwa kufunga goli tatu huku mwaka wa 2008 akiweka rekodi kama mchezaji aliyefunga magoli mengi. Baadae baada ya kuchezea Manchester united kwa mda, Cristiano Ronaldo alijiunga na Real Madrid huku club ya real Madrid wakilipa $131 million Kama ada ya uhamisho

Aliwahi kupata tuzo ya ballon d’or Mara tano mfululizo na kuiwezesha nchi yake ya Portugal kuwa washindi wa 2016 European championship. Mwezi wa July 2018, Ronaldo Alisajiliwa na club ya Juventus iliyoko Italy

picha za Cristiano Ronaldo

Maisha ya Cristiano Ronaldo

Ronaldo alizaliwa February 5 mwaka wa 1985 maeneo ya Funchal, Madeira, Portugal, kisiwa kidogo kilichoko Nchini Portugal. Cristiano Ronaldo ndiye mdogo kwenye familia ya watoto wa nne. Kaka zake ni pamoja na Maria Dolores, does Santos pamoja na josé dinis aveiro. Jina lake limetokana na muigizaji mashuhuri Ronaldo Reagan ambaye alikuwa kipenzi Cha Babake katika uigizaji.

Ronaldo alikulia kwenye familia ya kimasikini na yeye na familia yake walikuwa wakiishi kwenye nyumba ya mabati iliyokuwa karibu na bahari. Babake Ronaldo ndiye aliyemuunganisha na mchezo wa soka kwani alikuwa akifanya Kazi na club moja iliyojulikana kama boy’s club.

Maisha ya familia ya Ronaldo yalikuwa magumu sana kwani Babake alikuwa mlevi sana. Mamake Ronaldo alijitahidi sana ili kuweza kuwalea wanawe kwa kufanya Kazi ya kupikia watu na kuoshea watu nyumba na nguo zao.

Mwaka wa 2005 wakati Cristiano Ronaldo akichezea Manchester united Babake aliaga dunia baada ya kuugua magonjwa ya Figo yanayoletwa na ukunywaji wa pombe kupindukia.

Masaibu hayakukomea hapo kwani mwaka wa 2007, mamake alikuwa yuagua ugonjwa wa saratani. Maisha yalizidi kuwa magumu kwa Cristiano Ronaldo. Alipitia wakati mgumu Babake alipokufa kwani alikuwa mkaribu wake. Baada ya Babake kufa, historia ya Cristiano Ronaldo ilichukua mkondo mpya.

Katika maisha yake, Ronaldo alikuwa akimpa ushauri Babake atembelee kituo Cha rehab ili aweze kusaidika na labda aache ama apunguze kabisa kulewa Ila Babake hakuwa tayari kwa hayo.

Akiwa na miaka 10, tayari Cristiano alikuwa ashajulikana kama mwanasoka hatari sana aliyependa soka kiasi kwamba hata angesahau chakula na kulala. Katika uvulana wake alipenda kucheza mpira. Kulingana na Fernao Sousa aliyemlea baada ya Babake kuaga, Ronaldo angetokea dirishani kwenda kucheza mpira wakati alitakiwa awe ndani ya nyumba akifanya home work.

Kuna wakati Portugal iliwahi kuwa na mechi na Manchester united wakati huo Cristiano Ronaldo alikuwa bado hajajiunga na Manchester united. wachezaji wa Manchester united waliona uwezo wake mkubwa na kumsihi meneja wa club ya Manchester united kuongea naye iko ajiunge na club yao. Hii ilifanyika baada ya mda na Ronaldo akajiunga na Manchester united

Mwaka wa 2007, Ronaldo Alisajiliwa na Manchester united kwa mda wa miaka tano kiwango Cha pesa kikiwa £31 million.

Mwaka wa 2008, Ronaldo alijishindia tuzo kama mchezaji bora ulimwenguni Kulingana na FIFa. Aliiwezesha Manchester kuwa bingwa Mara tatu katika ligi ya premier.

Historia ya Cristiano Ronaldo

Cristiano Ronaldo akiwa real Madrid

Mwaka wa 2009, club ya real Madrid iliyoko Spain ilifikiana kumunua mchezaji huyu kutoka timu ya Manchester united kiwango Cha pesa kikiwa $131 million. Cristiano Ronaldo alikuwa na wakati mgumu sana kwani alipenda sana timu yake ya Manchester united. Wengi walishangazwa na Jambo hilo la Ronaldo kuhama kutoka Manchester united hadi Juventus.

” Najua club yangu mpya ya Juventus inatarajia nifanye makubwa zaidi na nifaulu na najua nitakuwa na wakati mgumu kuliko niliokuwa nao wakati nikiwa Manchester united kwani nimechezea Manchester united kwa miaka mingi… Najua nitakuwa na mtihani zaidi Ila hii itanisaidia kuwa mchezaji bora zaidi…”

Ronaldo alizidi kupata tuzo zaidi na heshima kwake ikazidi. December 2016, alishinda Ballon d’Or awards Mara ya nne na kueka rekodi mpya iliyowekwa na Lionel Messi hapo mbeleni.

Katika tuzo zenye Ronaldo alishinda mwaka wa 2016 ni pamoja na European championship, champions league, club world cup pamoja na individual awards kutoka UEFA pia France football magazine. Mwaka uliyofuatia, alishinda tuzo ya tano ya ballon d’or

Cristiano Ronaldo akiwa Juventus

Kulitokea fununu kwamba mda wa Ronaldo kuchezea Juventus ulikuwa umeisha. Hii ilikuja kuwa kweli July 2018 baada ya Cristiano Ronaldo kutangaza kwamba aliweka mkataba na Juventus club kutoka Italy baada ya Juventus kulipa $140 kama ada ya uhamisho.

Kupitia barua ya wazi, Ronaldo aliongea na mashabiki wake wa real Madrid na kusema haya;

” Nimekuwa na wakati mzuri sana na timu ya real Madrid.. najua hii ni klabu kubwa na naiombea.. kwa mashabiki wangu nawashukuru sana kwa mapenzi yenu mumekuwa nayo kwangu… “

Maisha ya Ronaldo akiwa Juventus yalifaulu sana kwani alifunga magoli kumi katika mechi 14 za kwanza aliiwezesha timu yake kushinda tuzo za serie A tittle mpaka akapewa jina la league’s MVP mwezi wa may 2019.

August 27 mwaka 2021, kulitangazwa kwamba Ronaldo alikuwa arudi Manchester united Ambapo anachezea kwa sasa.

Ronaldo akiwa Portugal timu ya nyumbani

Cristiano Ronaldo alikuwa captain wa timu kuu ya Portugal. Aliiwezesha timu ya taifa ya Portugal kufika final ya European championship na wakacheza na timu ya France.

Hata kama alitolea dakika ya 25 baada ya kuumia goti, timu ya Portugal ilipata ushindi wa goli moja kwa nunge na kupata tuzo la kimataifa. Wanatimu wenzake walimusifu Ronaldo na kusema kuwa yeye kama captain alichangia pakubwa sana kuweza kupata ushindi wa kimataifa.

Hayo ndiyo tupo nayo kwa Leo hapa mwangaza kuhusiana na historia ya Cristiano Ronaldo. Zidi kufuatilia habari zetu hapa mwangaza news ili uwe wa kwanza kuzipokea.

Soma hii pia : Historia ya Lionel Messi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *