HistoriaMaisha

Historia ya Onsongo comedian

Huku Tanzania wakiendelea kujivunia Mai zumo, Nchini Kenya wasanii wa kuchekesha wenye umri mdogo wanazidi kuchipuka. Alianza TT comedian na sasa Kuna Onsongo.

Kwa majina kamili Anajulikana kama Abraham Onsongo ila wengi wanamfahamu kama Onsongo comedian. Kwa sasa ameshika Kasi sana na anapatikana kwenye mitandao tofauti tofauti ikiwemo YouTube. Onsongo ameanza kuwa maarufu wiki chache zilizopita na wengi wakaanza kufuatilia vichekesho vyake.

Vichekesho vyake ni tofauti sana na lugha yake ya mama inachangia kuleta utofauti. Abraham Onsongo ni mzaliwa wa county ya Nyamira huko kisii na kwa vichekesho anaitumia lugha ya taifa ya kiswahili.

Kuzaliwa kwa Onsongo

Onsongo alizaliwa mwaka wa 2011, hii Ina maana mwaka huu wa 2021 ako na miaka kumi. Alizaliwa sehemu inayojulikana kama Rigoma, magambo katika county ya Nyamira. Amezaliwa na wenzake na kwa familia wako watoto watatu.

Masomo ya Onsongo

Kwa sasa ako grade 4 katika shule ya Zana junior academy iliyoko Gachoba, Rigoba county ya Nyamira. Anapenda kucheza soka akiwa shule.

Maisha ya Onsongo

Onsongo alianza vichekesho ndani ya kikundi cha inajoma comedy. Ifahamike kwamba, inajoma comedy actors ndio wanamsimamia katika shughuli zake zote kuhusiana na talanta yake ya vichekesho. Walipatana na kikundi hicho wakati inajoma comedy actors walikuwa wakitafuta waigizaji ama ukipenda auditions. Waliamua kumsaidia Onsongo na hata wakamfungulia youtu channel Onsongo comedy Ke

Onsongo hutengeneza video fupifupi baada ya kutoka shule na shule zikifungwa, Onsongo hutengeneza video za dakika zaidi. Kulingana na mahojiano ya hivi karibuni, Onsongo alieleza kuwa yeye hubuni vichekesho vyake mwenyewe. Kulingana na yeye, alizaliwa na talanta ya kuchekesha ni sio eti ameridhi ama kufundishwa na yeyote.

Ndoto za Onsongo

Onsongo angetaka kuwa mchekeshaji mkubwa akiwa mkubwa. Kwenye YouTube channel yake ako na zaidi ya subscribers elfu sabini. Amekuwa kwa media tour na juzi aliweza kufanya mahojiano na Lulu Hassan ndani ya Citizen Tv

Ni hayo tu hapa mwangaza news natumai umefahamu Mengi zaidi kuhusu osongo ni hii hapa ni video yake moja ya vichekesho

 

Soma hii pia: Historia ya Otis Flaqo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *