Adasa azidi kuwa tishio
ADASAAdasa azidi kuwa tishio; Sanaa,usanii ,tungo na msanii .Usanii nikipaji ambapo kila mmoja huwa na kipaji na hulka yake ya Usanii hutegemea Tu Sanaa yake itakua juu ya nini.
Haya basi Leo tuna mzungumzia mwanadada anaekuja Kwa Kasi Sana kiasi cha kuiteka mioyo ya WA Kenya wengi na watanzania Kwa ujumla nae simwengine ni ADASA.
Adasa ni mmoja WA wasanii wachache wanaofanya vizuri kimzki ,na mziki wake umekuwa ukiskizwa na watu wengi zaidi hii ni Kwa sababu ya tungo zake za mapenzi zinavyo ongoa wasikizaji nakupasua mioyo Yao Kwa furaha.
Mwanamziki huyu kutokea Kenya anaonekana kupitia upinzani mkubwa kwani wapo wasanii wakongwe zaidi yake wakike amboa pia nyota zao zangaa. Nyota ndogo,sanaipei tande na Nadia ni wasanii kutoka Kenya ambao wamekua wakimpa msanii adasa bumbuazi ju uimbaji wao.
Licha ya hayo adasa alituarifu kupitia mahojiano ya moja Kwa moja kua licha yakua anapitia upinzani mkubwa yeye hajawai kukata tamaa na badala yake anazidi kutoa mziki WA hadhi kila uchao,duru zilizotufika zinasema mwanamziki adasa amewashinda wasinii tajika nchini Tanzania ambako wako wasanii wanaowika.
Adasa amekua maarufu lakini siyo kwa uwepo wake pekeake Kwani ukiona cha Elea juwa kimuundwa ,nae Yuko chini ya usimamizi Wa Jos K madala studio yake yajiita dalaz record iko bamburi Mombasa .
Adasa anarekodi na producer mkongwe, Emmy d. Huyu pia ni producer tajika kwenye tasnia ya muziki kwani ameweza kuwafanyia wasanii wengine maarufu mbali na Adasa na mziki wao ukashika akiwemo dogo richie,sudiboy,rudeboyz, daddy sele,fat s na wengine.
Kunazo Kampuni mbali mbali pia hazikuachwa nyuma ziliipokea vilivyo sauti ya mwana dada adasa inavyovutia wakaamua wamtafute ili kufanya nae biashara
Kampuni ya “HEWA” ndio iliyo kuwa yakwanza kutaka kumpa matangazo kuyapeperusha hewani Kwa njia ya Sanaa ya uimbaji.
Licha yakuwa ni msanii Wakike hakuchukua taasubi yakike alijichanganya na wasanii wakiume ili kuboresha uimbaji wake Kwa ladha tofauti adasa alipiga colabo na mejja msanii kutoka Nairobi ambae pia yeye anafanya vizuri Kwa uimbaji ,nyimbo Yao inayojulikana kama ” najidai”
Adasa amejikakamua na hadi sasa ameachia nyimbo takriban nane ambozo ni;
- say yes – Adasa
- Tubanane – Adasa
- Mahaba Niue – Adasa
- Nipekeche – Adasa
- Tunaendana – Adasa
- Niloweshe – Adasa
- Noma – Adasa
Kiukweli zote zimefanya vizuri japo ipo iliyo zidi umaarifu ambayo ni “say yes”utunzi na mtiririko wa vina vilivyo bobea nahau na misemo iliupa wimbo huo umaarufu mkubwa .SAY YES.
Soma hii pia : jemutai amvua nguo prof Hamo
1,667 total views, 2 views today