Jemutai aongea mazito kuhusu prof Hamo
Jemutai aongea mazito kuhusu prof Hamo; Aliyekuwa muigizaji wa show ya churchill na mchekeshaji jemutai amefunguka na kusema kuwa mchekeshaji mwenza prof Hamo ndiye baba wa watoto wake wawili. Jemutai ameongezea kuwa prof Hamo amekataa katakata kusimamia majukumu ya watoto hao.

Ripoti hiyo imetolewa na Edgar Obare ambaye Kazi yake huwa ni kutoa siri kwa uma za watu sanasana walioko kwenye uhusiano. Jemutai ameeleza kwamba mtoto wao wa kwanza na prof Hamo walimpata mwaka wa 2016 naye mtoto wa pili ambaye ni msichana walimpata October 2019.

Kulingana na mchekeshaji huyo, uhusiano wake na Hamo umekuwa wa vuta ni kuvute. Kuna wakati Hamo aliwahi kumwambia jemutai aache Kazi ndani ya churchill ili waweze kukuza jina lake kama brand.
Uhusiano wa jemutai na prof Hamo ulijulikana alipomwambia Edgar Obare amsaidie jemutai kuiuza facebook account yake iliyoko na zaidi ya watu 850k. Sababu ya kuuza hii facebook account ilikuwa ni jemutai apate pesa ya kuwalea watoto wake na pia kulipa kodi ya nyumba anayodaiwa kwa miezi kadhaa.

” Kwa jina naitwa jemutai, mimi ni mchekeshaji na mama wa watoto wawili. Mimi ni single mother na vile maisha yamekuwa magumu, nadaiwa kodi ya nyumba kwa miezi kadhaa. Sina lingine la kufanya ila kuiuza facebook account yangu ambayo iko na watu laki nane na nusu. Nauza shilingi mbili kwa kila mfuasi ( follower) mmoja. Nikiuza hii facebook nitapata pesa ili niweze kufungua biashara ndio niweze kulea Watoto wangu…”
Jemutai amekili kwamba prof Hamo ako na mke mwingine nakuru anayempenda zaidi na pia jemutai anamjua na ashawahi msaidia wakati alikuwa na pesa. Jemutai amesema prof Hamo hatoi chochote kwa watoto wake bali na kufanya Kazi Hot96
Soma hii pia : historia ya Eric Omondi