MaishaSanaa

Historia ya Eric Omondi

Historia ya Eric Omondi; Eric Omondi ni muchekeshaji anayetokea nchini Kenya. Ni msanii anayependwa zaidi Nchini kenya, nchi jirani na ulimwengu mzima. Bali na kuchekesha, Eric Omondi pia ni emcee, mtangazaji na pia muigizaji.

Eric Omondi alizaliwa mwaka wa 1987 tarehe tisa mwezi wa March. Hii Ina maana mwaka huu wa 2021 ako na umri wa miaka 36. Alizaliwa nchini kenya sehemu inayojulikana kama Kisumu. Ni mjaluo kutoka Kisumu county na hivi majuzi serikali ya county ya Kisumu iliamua kuita barabara moja kutumia jina lake; ” Eric Omondi road”. Hii ilikuwa furaha kwake na aliwashukuru wahusika kwa kupewa hiyo heshima.

Eric Omondi ni kakake Fred Omondi ambaye pia ni mchekeshaji. Miaka kadhaa iliyopita walimpoteza kaka yao mkubwa kwa jina joseph kutokana na madawa ya kulevya.

Eric Omondi fred Omondi
Eric Omondi na kakake Fred Omondi

Eric Omondi alisomea shule ya msingi ya Kondelo kisha akajiunga na na shule ya upili ya Kisumu boys high school. Baadae alijiunga na Daystar university iliyoko athi river Nairobi ili kusomea mawasiliano.

Bali na uchekeshaji, Eric Omondi alisikika akisema kwamba alitaka kuwa mtangazaji. Aliwahi kupata Kazi ndani ya runinga ya NTV ila Kazi hiyo iliisha baada ya wiki mbili. Baadae alianza comedy na kujiunga na churchill aliyemsajili kwa show yake ya churchill show ndani ya NTV.

Baadae aliamua kufanya Kazi kivyake baada ya kuanza show yake KTN kwa jina “Hawayuni” show hiyo haikukaa sana kabla ya kusimamishwa kwani haikupata watazamaji wengi. Hii haikumvunja moyo kwani aliamua kuchukua mda wake ili kuelewa makosa yake na kuisoma Sanaa vizuri kabla ya kuendelea.

Ni hivi majuzi tu Eric Omondi aliachana na mpenzi wake wa miaka mingi Chantal Grazioli mzaliwa wa Italia. Wawili hawa walikutana wakati wa kenya at 50 show iliyofanyika kwenye uwanja wa kasaranieric Omondi wife Chantal

 

Kuliwahi tokea tetesi kwamba Eric Omondi na Jackie Maribe walikuwa wapenzi na pia wawili hawa wako na mtoto. Bado haijabainika wazi kama kuna ukweli kuhusiana na wawili hawa ama la. Inavyofahamika kwa Sasa ni kuwa Eric Omondi yupo “single”

Eric Omondi jackie maribe

Utajiri wa Eric Omondi

Utajiri wake unasemekana kuwa Kshs. 80 million. Bali na uchekeshaji, yeye huwa ambassador wa kampuni kadhaa kama vile OLX, Unga wa Dola, maziwa ya Loto, pekee tissue papers na zinginezo. Juzi alifungua studio yake mpya kwa jina Bigtyme Entertainment & Eric Omondi studios iliyoko Lavington. Studio hii ilianzishwa November mwaka wa 2020. Hapo ni ofisi yake na pia utayarishaji wa matangazo ya biashara (adverts) na mziki hufanyika hapo.

Soma hii pia ( historia ya Ben Githae)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *