InternationalMchipuko

Historia ya Purity Mwambia Guns Galore

Purity Mwambia ni mtangazaji wa citizen Tv. Ni mtangazaji anayejulikana kwa kufuatilia habari za kijasusi zenye watu wengi hawazijui na kuzieka wazi bila uoga wote. Kwa Mara nyingi amejikuta katika upande mbaya wa serikali kwa habari zake.

Ashatoa siri nyingi zinazofanyika nchini kenya ikiwemo hii ya majuzi ya “Guns Galore” iliyozua gumzo kwenye mitandao na vyombo vya habari.

Purity Mwambia alizaliwa na kulelewa ukambani nchini kenya. Kwa Sasa umri wake hajaueka wazi kwa mitandao ila ako Kati ya miaka 30-40.

Purity Mwambia amesomea na amehitumu utangazaji katika katika chuo kikuu tajika. Kila uchao purity Mwambia anazidi kuwa mkali zaidi katika taaluma yake ya utangazaji.

guns Galore purity Mwambia

Kazi yake ya utangazaji ilianzia katika Runinga ya KTN. Hapo alifanya Kazi kwa mda mrefu sana mpaka akapandishwa cheo na kuwa ripota mkubwa katika kitengo cha lugha ya kiswahili. Baadae alijiunga na kampuni ya media max na kufanya Kazi ndani ya K24. Akiwa K24 Tv aliwahi kufanya habari moja ya ujasusi iliyopandisha jina lake kwani ilipata utazamaji mkubwa nchini.

purity Mwambia biography

Miaka kadhaa baadae alijiunga na kituo Cha royal media na kuanza kufanya Kazi ndani ya Citizen Tv. Ndani ya Citizen amekuwa akipeperusha habari za ujasusi moja baada ya nyingine. Kati ya hizo habari ni Bweta la Uhalifu, Virusi safarini, na ya hivi karibuni kwa jina guns Galore. Kulingana na yeye, kufanya hizo taarifa yataka moyo kwani unaweza jikuta kwa mkono mbaya.

Kwa mfano, wakati purity Mwambia alikuwa K24, dereva mwenye alikuwa mmoja wao wakati wakifanya uchunguzi wa Bweta la Uhalifu alivamiwa na wahalifu waliokuwa wakitafuta habari kuhusu purity Mwambia. Kulingana na Mwangi aliyekuwa dereva, wahalifu hao walikuwa wanatafuta video footage zozote zilizohusu ujasusi wa purity Mwambia. Bweta la Uhalifu haikuwahi kuonyeshwa kwa runinga kwani mamlaka iliingilia Kati.

Guns Galore ya purity Mwambia ilionyeshwa tarehe 18 April 2021 ndani ya citizen Tv. Guns Galore ilikuwa ni kuhusu vile askari hufanya biashara na uniform zao, pingu na hata bunduki. Kulingana na ripoti yake, wanaokodisha vifaa hivo huvitumia kufanya uharifu. Hii imeacha wengi kinywa to wazi kwani bado haileweki vile Jambo kama hili laweza fanyika bila wizara ya ulinzi kujua.

Purity Mwambia anasemekana kuolewa ila bado haijajulikana wazi mume wake ni nani kwani anapenda maisha yake kuwa ya siri. Kazi ya purity Mwambia inampea pesa za kisawasawa na kwa Sasa utajiri wake unafikiriwa kuwa Kshs 100 million.

Soma hii pia ( historia ya Eric Omondi)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *