Mchipuko

Andrew Kibe aacha kazi Kiss FM

Mtangazaji wa kiss FM, Andrew kibe ameacha kazi. Akiongea na gazeti la kenyans.co.ke, mtangazaji huyo amesema leo jumanne tarehe 30 ndio ilikuwa siku yake ya mwisho kufanya kazi kiss FM inayomilikiwa na Radio Africa.

” Niliwajulisha wakubwa wangu kuwa nitaacha kazi miezi tatu iliyopita kwani nilikuwa nawekewa vikwazo vya chenye nastahili kuongea hewani…”

Andrew kibe Anajulikana kwa kuongea bila kuogopa na kwa sasa ameamua kurudi kwa mitandao ili kukuza jina lake zaidi.

Andrew kibe and kamene goro

“Katika mitandao naweza weka chochote nachokitaka na hakuna atakaye nizuilia. Kwenye mitandao hakuna mtu wa kunizuia…”

Ametoa shukrani kwa mwenzake kamene goro ambaye alikuwa mfanyi kazi mwenzake ambaye pia alifanya kazi naye NRG radio.

Andrew kibe sister

“Nashukuru kwa kufanya kazi na kamene goro na Nina uhakika karibuni atanifuata”

Kulingana na kampuni ya data ya Geopoll, show ya Andrew kibe na kamene goro, ilikuwa yasikizwa na watu zaidi ya laki saba. Show yao ilipata nafasi ya pili Kenya nzima after show ya maina and king’ang’i ndani ya classic Fm.

Andrew kibe car

Andrew kibe na kamene goro walianza kazi ya utangazaji ndani ya kiss tv mwaka wa 2019 baada ya kuacha kazi NRG radio. Show yao ilipata umaarufu kwani walikuwa wanaongelea mambo yanayotendeka kwenye jamii bila uoga.

Kibe atakuwa mtangazaji wa pili kuacha kazi baada ya jalang’o kujiondoa milele fm. Jalang’o pia alisema anataka kuendeleza YouTube channel yake huku akiahidi kutengeneza nafasi zaidi za kazi kwa watangazaji wenza.

Soma hii pia ( Ben Kitili waachana na Amina tazama sababu)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *