International

Anerlisa Muigai na Ben Pol mda mfupi kabla ya kuachana

Anerlisa muigai na Ben pol wamekuwa wakigonga vichwa vya habari baada ya habari kuwa wawili hawa wameachana. Kumbuka wawili hawa walifanya harusi ya siri katikati ya mwaka Jana.

Kwa sasa inaonekana habari za kuachana kwao zilikuwa za ukweli baada ya anerlisa kusema kwamba amekubali kutia sahihi talaka yake na Ben pol.

Wengi hawakudhania uhusiano wa wawili hao ungekatika mapema kwani wengi walitegemea Anerlisa Muigai na Ben pol kuishi maisha marefu pamoja na hata kuzaa watoto pamoja.

Tofauti zao zilianza kuonekana wakati wawili hawa waliacha kufutiliana katika mitandao yao ya Instagram mwezi wa agosti mwaka wa 2020. Hii ilionyesha wazi kuwa uhusiano wao ulikuwa unaelekea pabaya.

Siku chache baadae, Ben pol aliandika ujumbe ulioashiria kuwa kulikuwa na tatizo kwa ndoa yao na kusema; ” nataka kufanya usafi “. Wengi hawakuelewa ni kitu gani kilikuwa chaendelea na maisha ya Ben Pol

Miezi kidogo baadae, Anerlisa alijitokeza waziwazi na kusema yeye na Ben pol hawako tena kwenye uhusiano. Hii ni baada ya mashabiki wake wa Instagram kutaka kujua kitu gani kinaendelea Kati yake na Ben pol.

Aliongeza kusema kwamba yeye hapendi mtu yeyote ambaye Nia yake ni kumharibia jina ama mtu mwenye hampi heshima. Aliendelea kusema kwamba Kuna Jambo Ben pol alimfanyia ambalo halikumpendeza

Mwezi wa October 2020, Ben pol alibadilisha dini na kuwa muisilamu. Jambo hilo lilishangaza wengi ikizingatiwa yeye na mke wake anerlisa muigai walifanya harusi ya ki kristo tena kanisani. Hii tayari ilionyesha wazi kwamba Kuna kitu hakiendi sawa Kati ya wawili hawa.

Kwa mda huo, wawili hawa hakuna aliyekuwa alipost mwingine kwa mitandao ya kijamii.

Soma hii pia: wa kufanya tendo la ndoa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *